Friday, 16 June 2017

Waziri wa Tamisemi atoa onyo hili kwa wakuu wa mikoa na wilaya

Dodoma. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia vibaya madaraka yao ya kukamata watu walio kwenye himaya zao.

Ametoa onyo hilo leo (Ijumaa) alipojibu maswali ya wabunge waliotaka kufanyika marekebisho ya sheria inayowapa mamlaka wakuu hao ya kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wanaowatuhumu kwa lolote.

Licha ya kubainisha kwamba sheria hiyo haina tatizo, waziri amesisitiza: "Ukamataji unatakiwa ufanywe kwa mtu aliyetenda kosa la jinai au anayehatarisha usalama. Isiwe kwa show-off tu. Na mhusika anatakiwa kufikishwa mahakamani mara moja, asishikiliwe tu."

Amesisitiza kwamba wakuu hao ni wawakilishi wa Serikali kwenye maeneo yao, hivyo hawatakiwi kutumia vibaya madaraka waliyokasimiwa.

Katika siku za karibuni wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakilalamikiwa kuwaweka watu kizuizini pasipo kuwa na sababu za msingi, miongoni mwao wakiwamo waandishi wa habari.

Related Posts:

  • Rwanda yaitoza MTN faini ya dola milioni 8 Kampuni kubwa ya mawasiliano ya MTN tawi la Rwanda imetozwa faini ya zaidi ya dolla milioni 8 za Marekani kwa kile kilichotajwa kuwa kukiuka makubaliano baina yake na serikali ya nchi hiyo. Kampuni hiyo yenye wateja takrib… Read More
  • Tamko la mradi wa bomba la mafuta ghafi lasainiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima… Read More
  • Trump kuzuru Israel chini ya ulinzi mkali Rais wa Marekani Donald Trump anazuru Israel na Maeneo ya Wapalestina leo, akiendelea na ziara yake ya kikazi katika maeneo ya Mashariki ya Kati. Atafika maeneo hayo akitokea Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani, amba… Read More
  • Libya yakabiliwa na vita vya ndani Taarifa kutoka nchini Libya zinaelez kwamba jeshi liloljitangaza kuwa la taifa hilo, ambalo linaunga mkono mamlaka yenye makao yake katika mji wa mashariki wa Tobruk,limefanya mashambuliuzi kadhaa ya anga dhidi ya vikosi pi… Read More
  • Mwanamke akata uume wa kiongozi wa dini India   Mwanamke mmoja wa umri wa miaka 23 nchini India amekata uume ya wa kiongozi mmoja wa dini kwenye jimbo lililo kusini mwa nchi la Kerala, akidai kuwa alimbaka kwa miaka kadha. Polisi wanasema kuwa kiongozi huyo wa d… Read More

0 comments:

Post a Comment