Watoto wawili wameripotiwa kufariki huku watu wengine watatu wakiwa wamejeruhiwa baada ya shambulizi la bomu kutokea Nigeria.
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na polisi wa Adamawa ni kwamba mtu asiejulikana aliingia katika kijiji cha Rake akiwa na gari na kuwapa watoto wawili mkoba akiwataka waupeleke nyumbani.
Ripoti zinaonyesha kuwa mtu huyo aliwaambia watoto hao kuwa ndani ya mkoba huo kuna vitu vya thamani na fedha hivyo wahakikishe wanaufikisha nyumbani salama.
Watoto hao waliupeleka nyumbani na ghafla mkoba ulilipuka na kusababisha vifo vya watoto wawili huku watu wengine watatu wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Uchunguzi zaidi wa aliyesababisha shambulizi hilo unafanyika.
Saturday, 10 June 2017
Home »
» Shambulizi la bomu lasababisha vifo vya watoto wawili Nigeria
0 comments:
Post a Comment