Mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amewataka wapenzi wote wa muziki waweze kumbeba ili asipotee tena kama ilivyokuwa hapo awali baada ya kukosa sapoti pamoja na ukosefu wa fedha.
Saida amesema baada ya kupata matatizo ya ukosefu wa fedha ikiwa ni baada ya mtafaruku kati yake na uongozi aliokuwa nao awali kwa sasa anahitaji sana msaada wa watu wengi zaidi ili aweze kukaa sawa katoka muziki.
“Nimerudi rasmi kwenye muziki wangu, Nibebeni maana mimi ninabebeka, wapenzi wa muziki wa Saida nipokeeni kwa mikono miwili ili niendelee kuwepo,” Saida alikiambia kipindi cha EATV. “Lakini nawaomba wafadhili mbalimbali waweze kujitokeza ili kunipa msaada wa mahitaji nizidi kuwepo. Pia nimewaandalia mambo mazuri kwenye albamu yangu ambayo nitaizindua tarehe moja nimeshirikiana na wasanii kibao akiwepo G nako pamoja na Belle9” alisema Saida Karoli.
Kuhusu kuendelea na muziki wa asili Saida amesema kwamba muziki wake japokuwa una vionjo vya kisasa lakini hawezi kuuacha muziki wa asilikwani ndiyo uliomtambulisha na kumpatia mashabiki wengi ndani na nje ya Africa.
0 comments:
Post a Comment