Tuesday, 13 June 2017

Alichosema Zitto Kabwe baada ya ripoti ya madini

"Mwisho wa siku historia inaandikwa tu. Uzalendo ni kufanya jambo ambalo wengi hawakuelewi lakini wewe unajua Ni jambo sahihi na unakubali kutukanwa, kususubikwa, kusimangwa, kuzushiwa, nk. Unapambana tu. Mwisho wa siku waliokuita msaliti watakuita shujaa. Waliokuzomea wanashangilia. Wewe unafanya nini? Unakaa kimya kwani kwenye kukaa kimya pia kuna kusema kukubwa zaidi. Muhimu Nchi ifaidike. 

Huko nyuma nilipata kusema, hata mungu akinichukua sasa unakwenda ukiwa umetabasamu kwani unakuwa umetimiza wajibu wako duniani. Kina Josina Umm Kulthum wataishi Kwa heshima inshallah" Ameandika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook mara baada ya ripoti ya pili ya mchanga wa madini kuwasilishwa

0 comments:

Post a Comment