Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amehukumia kifungo cha siku 30 jela kwa kukiuka sheria baada ya kuandaa maandamano
Alikamatwa nyumbani kwake mjini Moscow siku ya Jumatatu kabla ya kufanyika kwa maandamano ya kupinga ufisadi nchini Urusi.
Mamia ya watu walikamhwa wakati wa maandamano hayo yaliyofanyika kote nchini.
Polisi wa kupamba na maandamano walikuwa wakiwakamata waandamanaji kutoka kwa umati, kwa mujibu wa mwandjshi wa BBC aliyekuweko.
Mahakama ya Moscow iltangaza umuzi wake jana Jumatatu na kukataa wito wa mawakili wa Navalny kufuta kesi hiyo.
Kiongozi huyo wa upinzani mwenyr umri wa miaka 42 baadaye alithibitisha hukumu yake katika mtandao wa twitter.
Polisi mjini Moscow wanasema kuwa takriban watu 5000 walishiriki maandamano hayo mjini humo.
0 comments:
Post a Comment