Wednesday, 7 June 2017

Raia kulipwa kuuwa panya Mynmar

Panya wavamizi
Image captionPanya wavamizi
Maelfu ya panya wamevamia vijiji kadhaa katika manispaa ya mji wa Nga Pu Taw, kusini magharibi mwa jimbo la Ayeyarwady nchini Mynmar.
Vyombo vya habari nchini humo, vinasema kuwa vyakula na mimea mashambani imevamiwa na kulazimu mamlaka kuu nchini humo kuamua kuwalipa wananchi senti 4 kwa kila panya atakayeletwa kwa mamlaka akiwa ameuwawa.
Wanakijiji katika eneo la Ayeyarwady wamekuwa wakikabiliana na uvamizi huo wa panya kwa kuwaulia mbali wanyama hao ambao wamewavamia kwa wingi katika kipindi cha siku kumi zilizopita.
Maafisa wakuu wa eneo hilo wamelaumu mvua kubwa inayonyesha kwa sasa, jambo lililosababisha ongezeko kubwa la panya, huku wakivamia hifadhi ya chakula katika maghala ya wanakijiji.
Panya wengi wamepatikana kwenye nyumba 20, zilizoko karibu na vijiji vya Zee Chai village pwani ya manispaa ya Nga Pu Taw.
Kufikia sasa panya 800 wameuwawa, huku waliosalia wamekimbilia msitu ulioko karibu.
Wanakijiji nchini Mynmar wakisaka Panya
Image captionWanakijiji nchini Mynmar wakisaka Panya
Hayo ni kwa mjibu wa wakaazi wa eneo hilo.
Wananchi wanahofia kupatwa na maradhi yanayosababishwa na panya.
Ili kubaini ikiwa panya hao wana virusi vya ugonjwa mmbaya na bakteria acteria, panya wanaokamatwa wakiwa hai au waliokuwa hupelekwa kwenye maabara ya idara ya afya iliyoko mjini Yangon, hayo ni kulingana na idara ya afya katika jimbo hilo la Ayeyarwady.
Kwa mjibu wa Wizara ya Habari, panya wengi pia wameonekana wakiingia katika vijiji vya kisiwa cha Haigyi, mahali ambapo zaidi ya panya 1,600 wameuliwa.
Mnamo mwaka 2004, panya walivamia na kula kila kitu katika kijiji cha Pathein, makao makuu ya jimbo la Ayeyarwady, kutokana na ukosefu wa chakula, lakini hakuna aliyeambukizwa maradhi yatokanayo na panya.

0 comments:

Post a Comment