Tuesday, 13 June 2017

Panama yakata uhusiano na Taiwan na kuipendelea China

Picture of China's foreign minister Wang Yi (right) toasting Panama's foreign minister Isabel Saint Malo de AlvaradoHaki miliki ya pichaCHINA NEWS SERVICE
Image captionMawaziri wa Panama na Taiwan
Panama imekata uhusiano wake wa muda mrefu na Taiwana na badala yake imeboresha uhusiano na China
Serikalia ya Panama ilisema inatambua kuwa kuna China moja na hivyo inatambua Tawan kuwa sehemu ya China,
China inataja Taiwan kama mkoa wake ulijitenga ambao inasema unahitaji kuunganishwa nao.
Serikali mjini Taipei, mji mkuu wa Taiwan, imesema imekasirishwa na hatua hiyo ya Panama kujenga uhusiano na Beijing, lakini ikasema haitashindana na China katika kile ilichokitaja kuwa mchezo wa pesa katika diplomasia.
Chinese container ship in the Panama CanalHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMfereji wa Panama hutumiwa kwa wingi kwa biashara ya dunia
China ambayo hutumia pakubwa mfereji wa Panama kwa safari za meli, imeongeza kiwango cha uwekezaji wake katika taifa hilo la Amerika ya kati katika miaka ya hivi karibuni.
Mwezi Disemba mwaka uliopita kisiwa cha Sao Tome kilichukua hatua kama hiyo. Kwa sasa ni nchi 29 tu zimedumisha uhusiano wao na Taiwan.
Kufuatia tangazo hilo la Panama, vyombo vya habari nchini China vilichapisha picha za mawaziri wa nchi za kigeni wa nchi hizo mbili wakiweka sahihi.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China katika taarifa, ilisema kuwa serikali ya China inakaribisha hatua hiyo ya Panama.
Map of TaiwanHaki miliki ya pichaAP
Image captionTaiwan


source:bbc

0 comments:

Post a Comment