Friday, 16 June 2017

Kikwete uso kwa uso na Kardinali Pengo Dubai

Dar es Salaam. Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo.

Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.

Ingawa hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.

“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.” Ameandika Kikwete

Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.

Related Posts:

  • Ajinyonga kisa ugumu wa maisha Kijana Paulo Ezekiel, amejinyonga kutokana na kile kinachodaiwa ugumu wa maisha.Paulo (17) alikuwa anaishi na wazazi wake Mtaa wa Mazinge Kata ya Ndembezi mjini Shinyanga, alifariki dunia juzi usiku kutokana na kudaiwa kuji… Read More
  • Watetezi watatu kulitetea Gazeti la Mawio BARAZA la Habari (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Umoja wa Vilabu vya Habari Tanzania (UTPC) vinakusudia kufungua kesi kwenye mahakama kupinga uamuzi wa serikali wa kulifunga gazeti la Mawio. Se… Read More
  • Vigogo wawili Waliotajwa Ripoti ya Makinikia wamwaga fedha Kanisani WABUNGE watatu, wakiwamo Andrew Chenge na William Ngeleja ambao Kamati ya pili ya Rais kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusiana na makinikia Jumatatu iliyopita ilishauri wachunguzwe, jana walitoa mchango kwa k… Read More
  • Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ahamia K. Kusini kwa kuogelea Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ametorokea Korea Kusini kupitia kuvuka mto Han kwa kuogelea ,ikiwa ni mara ya pili kwa raia wa taifa hilo kuhamia kwa majirani zao.Mkuu wa Jeshi nchini Korea Kusini amesema kuwa mwanajesh… Read More
  • Mawaziri wawili wabanwa CHAMA cha ACT-Wazalendo kimelaumu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kufuatia kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kutawanya ma… Read More

0 comments:

Post a Comment