Kama kuna kitu kinawakera mashabiki wa Real Madrid baasi ni mtu anayeitwa Gerard Pique, mlinzi huyu wa kati wa Barcelona amekuwa hawezi kuikalia kimya Real Madrid hata kama wamefungwa au wameshinda.
Baada ya Real Madrid kufanikiwa kutetea ubingwa wa champions league wiki iliyopita walipongezwa na kila mtu ikiwemo klabu ya Barcelona ambao ndio waajiri wa beki huyo, kupitia Twitter Barca waliwapongeza Real Madrid.
Lakini kama ulidhani Barcelona kuipongeza Madrid ni Barcelona wote baasi umekosea sana kwani kwa Pique ni tofauti sana na anaona hakuna kitu na walichofanya Madrid hakiwafanyi kuwa bora kuliko wao.
Akiongea na kituo kimoja cha habari nchini Hisapania Pique amesema Real Madrid hawawezi kuigusa Barcelona hata kidogo “huwezi kufananisha walichoshinda katika miaka ya hivi karibuni na kile ambacho sisi tumeshinda”
Pique amewachana Real Madrid kwa kufanya bus parade akisema Real Madrid ni kawaida yao kusumbua watu na parade hizo wanapobebe ubingwa, akikumbushia mwaka 2011 ambapo Real Madrid walifanya bus parade walipobeba kombe la Copa del Rey.
Pique anaona hicho ndio kinawatofautisha wao na Real na ndio maana wao Barcelona wamebeba Copa Del Rey lakini hawakuona sababu ya kufanya “bus parade” kwani hawakutaka kuwasumbua watu na kombe dogo kama hilo lakini Real wangefanya hivyo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Pique kuishambulia Real Madrid kwani kama unakumbuka hata katika mchezo kati ya Real Madrid na Bayern Munich Pique aliiponda Real Madrid kwa kuwaambia wanabebwa sana na waamuzi.
SOURCE:MUUNGWANA
0 comments:
Post a Comment