Tuesday, 13 June 2017

Amri ya Trump kuzuia raia kutoka nchi za kiislamu yapata pigo jingine mahakamani

TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump alipiga marufuku baadhi ya raia kutoka nchi za kiislamu kuingia Marekani
Mahakama ya rufaa nchini Marekani imemua kuwa uamuzi wa kuzuia mpango uliofanyiwa marekebisho wa marufuku ya Rais Donald Trump kuzuia watu kutoka nchi sita za kiislamu utasabaki kuwepo
Wakitoa hukumu kufuatia kesi iliyowasilishwa na hjimbo la Hawaii, majaji walipata kuwa amri hiyo kuiu inakiuka sheria zilizopo za uhamiaji.
Rufaa hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Fransisco, ni kufuatia umamuzi uliotolewa kupinga raia wengi wao wakiwa kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani.
Hata hivyo mahakama haikusema kuwa serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi kwa watu wanaoingia nchini humo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa rais Trump,akisistiza kuwa kila lilalowezekana linatakiwa kufanywa kwaajili ya ulinzi wa Marekani
"Nadhan wote tunafahamu kuwa hizi ni nyakati za hatari dhidi ya tishio la ugaidi,tunapaswa kuwa kulinda kuingia kwa watu wanaoweza kufanya vitendo vya ugaidi na uwagaji wa damu.Tunaendelea kuwa na Imani kwamba amri za rais wetu ni kwa mjibu sheria na kwamba tunaamini mahakama ya juu itazipitisha"
Trump
Image captionTrump alipiga marufuku baadhi ya raia kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani
Hata hivyo mwanasheria mkuu wa jimbo la Maryland na Columbia Brian Frosh amefungua mashitaka dhidi ya rais Trump kwa madai ya kupokea malipo ya nje kupitia makampuni yake.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, Frosh Mwana Maryland's Attorney Generel, Brian Frosh, ameseama Trump kujihusisha biashara akiwa madarakani ni kuvunja katiba
"Aliiteuwa Hoteli yake ya kimataifa ya Trump kwaajili ya wanadiplomasia na maofisa wa serikali. Amekuwa akionekana kwenye sehemu nyingi za biashara zake na imekuwa kama sehemu ya kutangaza biashara hizo.Analipwa na makampuni yanayo milikiwa na nchi za nje kama vile China ambao pia ni wapangaji katika majengo yake.Na amekuwa akiendelea kuchukua malipo kutoka nchi za Saudi Arabia, India, Afghanistan na Qatar nchi ambazo zina hisa majengo yake ya kibiashara yajulikanayo kama Trump World Tower.
Trump
Image captionBaadhi waandamanaji wakipinga hatua ya Trump kupiga marufuku raia kutoka baadhi ya nchi za Kiislam kuingia Marekani
Rais Trump amekuwa akikabiliwa na upinzani mkali kufuatia baadhi ya maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya tangu kuingia madarakani,ikiwemo hatua hii aliyoichukua kupiga marufuku raia kutoka baadhi ya nchi za Kiislam kuingia Marekani.
source:bbc

Related Posts:

  • Trump asababisha Al Jazeera kufungiwa Saudi Arabia Saudi Arabia imeifungia mitandao ya Al Jazeera na Magazeti ya Qatar baada ya Rais wa Qatar Tamim Bin Hamad Al-Thani kusema anaishangaa Saudi Arabia kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kauli iliyopingwa na Mfalme wa … Read More
  • Ratiba ya Sportpesa Super Cup Sport Pesa Cup 5/6 Singida united Vs FC leopardYanga Vs Tusker fc6/5 Simba Vs Nakuru All StarJang`ombe boys vs Gor mahiaNusu fainali tarehe 8Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya… Read More
  • Nikki wa Pili ampongeza Rais Magufuli Msanii wa Nikki wa Pili, amempongeza Rais Magufuli kwa kitendo alichokifanya leo cha kumtumbua Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo na kumwambia Mungu amsimamie katika kupambana na ufisadi.Niki ameto… Read More
  • Kutana na Msikiti unaojengwa ila mafundi hawaonekani Uliwahi kusikia jengo linalojengwa kwa muda mrefu zaidi na mafundi hawaonekani, iwe usiku au mchana jengo linazidi kupanda juu, pia ata magari ya kubeba kokoto, mchanga hata matofari yasionekane...!!! Hii ni mpya kutok… Read More
  • Nape amposti Rais Magufuli na kuandika Ujumbe huu Mbunge wa Mtama mapema leo hii baada ya Rais John Magufuli kumfuta kazi Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospita Muhongo kutokana na wizara yake kutowajibika na kashafa ya Makontena ya Mchanga wa w Dhahabu. Rais Mag… Read More

0 comments:

Post a Comment