Wednesday 14 June 2017

BAADA YA KUISHINDWA KOREA KASKAZINI:Marekani kuwawekea vikwazo washirika wa kibiashara wa Korea Kaskazini

Rex Tillerson speaks at the Senate Foreign Relations Committee hearing in Washington. Photo: 13 June 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRex Tillerson
Marekani inasema itaziwekea vikwaza nchi ambazo zinafanya biashara haramu na Korea Kaskazini, kwa mujibu wa waziri wa mashuri ya nchi za kigeni Rex Tillerson
Alisema kuwa Ikulu ya White House hivi karibuni itaamua ikiwa itaziwekea vikwazo nchi hizo.
Utawala wa Trump umeamua kuiwekea shinikizo zaidi Korea Kaskazini kufuatia na mpango wake wa nuklia.
Majaribio ya makombora ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini ambayo yamepigwa marufuku naa Umoja wa Mataifa yamezua shutuma za kimataifa.
Korea Kaskazini inaaminiwa kupiga hatua katika kuunda makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kufika nchini Marekani.
North Korea's missile test. Undated photoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini inaaminiwa kupiga hatua katika kuunda makombora ya masafa marefu
Onyo la Bwana Tillerson lilitolewa wakati wa kikao cha bunge kuhusu mahusiano ya ya kigeni siku ya Jumanne.
Marekani haina uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini na imekuwa ikitoa vitisho vya kuyawekea vikwazo mataifa ambayo yanafanya biashara na taifa hilo.
Hata hivyo Bwana Tillerso hakuzitaja moja kwa moja nchi hizo.
Alisema kuwa suala la Korea Kaskazini litazungumziwa na China, mshikika mkubwa wa Korea Kaskazini wakati wa mazungumzo wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment