Saturday, 17 June 2017
Home »
» Kisa cha Polisi kuwapiga Mabomu ya Machozi Walemavu Dar
Kisa cha Polisi kuwapiga Mabomu ya Machozi Walemavu Dar
POLISI jana walitumia mabovu ya machozi kutawanya watu wenye ulemavu waliokuwa wamekusanyika na kufunga barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.
Mabomu hayo yalizua taharuki kwa watumiaji wa njia hiyo na kusababisha usumbufu kwao uliodumu takriban dakika kumi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, aliliambia Nipashe jana kuwa polisi walilazimika kutumia mabomu kama njia ya kuwakamata watu hao.
Kamanda Hamduni alisema kutokana na kitendo hicho, polisi wanawashikilia watu 40 akiwamo mwanamke mmoja.
Alisema lengo la mkusanyiko huo ulikuwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya kukamatwa na askari polisi wa usalama barabarani.
“Ni kweli tunawashikilia watu 40 akiwamo mwanamke mmoja kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
“Watu hawa walikuwa wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kupeleka malalamiko yao kuhusu kitendo cha kukamatwa na askari wa usalama barabarani,” alisema.
Kamanda Hamduni alisema baada ya polisi kufika eneo hilo na kutoa amri mara tatu ya kuwataka kutawanyika, walemavu walikaidi ndiyo maana waliamua kutumia mabomu ya machozi.
Alisema nguvu hiyo ya kutumia mabomu ilikuwa na lengo la kurahisisha ukamataji wa watu hao waliokaidi amri ya polisi kutawanyika.
SOURCE:MUUNGWANA
Related Posts:
Bintiye Mugabe ateuliwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habariHaki miliki ya pichaAFPImage captionBi Chikore alihitimu katika chuo kikuu Singapore Binti wa kipekee wa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Bona Mugabe-Chikore, ameteuliwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habari na sekta ya f… Read More
Ripoti ya Madini:Rais Magufuli amshauri Waziri ajiuzuluHaki miliki ya pichaGOOGLEImage captionRais wa Tanzania, Dr John Magufuli Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemshauri waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ajiuzulu. Hii leo Magufuli alikua akipokea taarif… Read More
Polisi 4 wauawa katika mlipuko Garissa KenyaHaki miliki ya pichaEPAImage captionMaafisa wa usalama katika shambulio la 2015 ambapo watu 147 waliuawa katika shambulio la al Shabaab dhidi ya chuo kikuu cha Garissa Kenya Maafisa 4 wa polisi wameuawa na wengine 4 kujeruhiw… Read More
RASMI:Magufuli amfuta kazi waziri wa nishati na madini Tanzania Sospeter MuhongoHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA Rais wa Tanzania John Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo. Taarifa kutoka ikulu imesema uamuzi huo wa Rais umeanza kutekelezwa mara moja, na kuwa nafas… Read More
Trump anakutana na Papa Francis VaticanHaki miliki ya pichaAFPImage captionRais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliwasili Roma Jumanne Rais Donald Trump anatarajiwa kuzungumza na Papa Francis na viongozi nchini Italia mjini Roma katika awamu ya tatu ya ziara … Read More
0 comments:
Post a Comment