Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na kibali.
Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alimemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Akisoma hati ya mashtaka, Mlay alidai kuwa Mei 19, 2017 huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji, Marco akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini bila kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi.
Marco katika shtaka la pili amedaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akifanya kazi kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.
Katika shtaka la tatu, Mlay alidai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).
Wakili Mlay alisema kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Marco kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 20 milioni na alikamilisha. Kesi imeahirishwa hadi Juni 21, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
Wednesday, 7 June 2017
Home »
» Mwanasheria Mkuu wa TBS Afikishwa Mahakamani
Mwanasheria Mkuu wa TBS Afikishwa Mahakamani
Related Posts:
- Mbasha ahofia kupata shambulio la moyo. MWIM-BAJI wa Mu-ziki wa Injili, Emmanuel Mbasha ameibuka na kusema kuwa amekubaliana na yote kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha ili kuepuka yaliyompata mzazi mwenzake na Zari, Ivan Ssemwanga wa Uganda ya kufariki dunia kwa s… Read More
- Islamic State yakiri kufanya shambulio Londona Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi London Polisi nchini Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi ambapo watu saba … Read More
- Jeneza la mwili wa Ndesamburo lazuiwa kupitishwa barabarani Moshi. Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro… Read More
- Ronaldo ameithibitishia dunia Ubabe wake!!! Cristiano Ronaldo ameithibitishia dunia yeye ni mchezaji wa aina yake baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitano mfululizo. Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid … Read More
- MAUMIVU KWA WOLPER: Harmonize amuonesha mpenzi wake mpya Huyu ndye Mpenzi mpya wa Harmonize Baada ya kuachana na mrembo wa filamu Tanzania Jacqueline Wolper, muimbaji wa wimbo Happy BirthDay kutoka WCB, Harmonize, ameonesha picha ya mpenzi wake mpya mzungu pamoja n… Read More
0 comments:
Post a Comment