Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameitaka Serikali kumjumuisha Rais Mstaafu kwenye tuhuma za Makontena ya Mchenga wa Dhahabu,
Akichangia bungeni katika hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18, Lissu amesema kuwa wakati wa kusaini mikataba ya madini Kikwete alikuwa ni Waziri wa Maji, Nishati na Madini.
“Katika taarifa hii ya jana wamependekeza watu fulani fulani washtakiwe makamishna, mwanasheria mkuu, Chenge (Mbunge wa Bariadi Andrew), Ngeleja (Wiliam- Sengerema) jamani naombeni niwaambie kitu ili wabunge muwe na maarifa,”amesema na kuongeza:
“Mtu wa kwanza kusaini mikataba na leseni za madini alikuwa ni Meja Jakaya Mrisho Kikwete, Agosti 5 mwaka 1994 alisaini leseni ya Bulyankulu inayopingwa leo hii wakati akiwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini wakati huo hakuwa na kinga ya urais.”
Amesema wakati aliposaini leseni na mikataba hiyo alikuwa hana kinga kwa masuala ambayo aliyafanya.
“Rais (Kikwete) alisaini si ya Bulyankulu pekee ya Nzega, ya Geita hizo leseni zina saini ya Kikwete anaponaje kwa mapendekezo haya? Anaponaje kama kweli mnataka kuwashughulikia watu walioshiriki kwenye mambo haya?”amehoji.
“Mbona mnachagua chagua hizi? Leseni na hizi sheria tangu mwaka 1999 tumesema tatizo kubwa ni sheria.”
Amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kama anataka kukumbukwa wakati wa uongozi wake basi asikubali kupitisha miswada ya sheria kwa hati ya dharura.
Akijibu swali hilo, Ndugai amesema atairuhusu miswada hiyo ya madini na gesi iingie bungeni kwa hati ya dharura.
“Kwanza wanaoamua siyo mimi tu ni kamati ya uongozi ya Bunge, lakini kama itakuja kwa hati ya dharura hii (madini) itaruhusiwa kwasababu moja tu tunaibiwa sana.” amesema.
Wednesday, 14 June 2017
Home »
» Lissu Amtolea Uvivu JK kuhusu kusaini mikataba ya Madini
0 comments:
Post a Comment