Wednesday, 14 June 2017

Muasi Bosco Ntaganda kutoa ushahidi

Bosco Ntaganda maarufu 'Terminator'Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBosco Ntaganda maarufu 'Terminator'
Aliyekua kiongozi wa waasi nchini Congo, Bosco Ntaganda anatarajiwa kutoa ushahidi leo katika mahakama ya kimatafa ya ICC.
Ntaganda aliyepewa jina la 'The Terminator ' atasimama kizimbani ikiwa ni takriban miaka miwili baada ya kesi kuanza.
Ntaganda anashutumiwa kutekeleza uhalifu na uhalifu dhidi ya binaadam unaodaiwa kutekelezwa na vikosi vyake.
Mashtaka yanasema kuwa kati ya mwaka 2002 na 2003 vikosi vyake vya uasi walivamia eneo la Ituri, wakatekeleza mauaji na vitendo vya kuwabaka raia.
Mwaka 2015, alikutwa na hatia kwa makosa 13 ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwasajili watoto wa umri wa chini ya miaka 15 kwenye jeshi na makosa mengine ya uhalifu dhidi ya binaadam.
Jopo lake la utetezi limepanga kuwaita mashuhuda 109 na wataalam wanne.Hii ndio sababu kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa.
Ikiwa atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 30 gerezani.

Related Posts:

  • Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani Sambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani. Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avas… Read More
  • Dawa za kupunguza makali ya HIV Watafiti nchini Uingereza wanasema dawa za kupunguza makali ya virusi katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini zimeboreshwa kiasi kwamba watu mwenye Virusi vya UKIMWI wanaweza kuishi kwa karibia sawa tu na watu wengine wasio na… Read More
  • Korea Kaskazini: Tuko tayari kuzungumza na rais Trump Korea Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira yataruhusu ,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini. Mjumbe mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na serikali ya rais Trum… Read More
  • Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey Rais wa Marekani Donald Trump amemtahadharisha mkuu wa shirika la uchunguzi wa jinai FBI aliyefutwa kazi James Comey dhidi ya kufichua habari kwa vyombo vya habari. Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Comey heri "a… Read More
  • Msichana wa Chibok akataa kurudi nyumbani Wasichana wa Chibok Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria. Alitarajiwa kuwa miongoni… Read More

0 comments:

Post a Comment