UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya kukitumikia msimu ujao kwa kutoa sharti moja kubwa ambalo ni klabu hiyo kumpatia shilingi milioni 70.
Mkude kwa sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya mkataba wake na Simba kudaiwa kumalizika hivi karibuni, ikiwa ni mwisho wa mkataba wake wa shilingi milioni 60 aliosaini kuitumikia Simba miaka miwili iliyopita.
Akizungumza kiungo huyo, amesema atakuwa tayari kusaini mkataba na klabu ya Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 kwenda juu kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa. Simba wamempa ofa ya milioni 40-50 ila yeye amekataa kwa kigezo kwamba mkataba unaoisha walimpa milioni 60 kwa sasa lazima dau lipande.
“Kwa upande wangu nipo tayari kutua Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 na kuendelea hadi shilingi milioni 150 na siwezi kusaini chini ya hapo, nipo tayari kutua katika timu yoyote kwa kiasi ambacho tutakubaliana kwa kuwa kiwango changu kipo vizuri.
Nahodha huyo wa Simba amesema lolote linaweza kutokea kuanzia sasa: “Tusubiri kila kitu kitakuwa wazi muda si mrefu na wadau watajua nitasaini wapi kwa ajili ya msimu ujao, wasiwe na hofu.”
Saturday, 10 June 2017
Home »
» Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga
Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga
Related Posts:
Kutana na Msikiti unaojengwa ila mafundi hawaonekani Uliwahi kusikia jengo linalojengwa kwa muda mrefu zaidi na mafundi hawaonekani, iwe usiku au mchana jengo linazidi kupanda juu, pia ata magari ya kubeba kokoto, mchanga hata matofari yasionekane...!!! Hii ni mpya kutok… Read More
Trump asababisha Al Jazeera kufungiwa Saudi Arabia Saudi Arabia imeifungia mitandao ya Al Jazeera na Magazeti ya Qatar baada ya Rais wa Qatar Tamim Bin Hamad Al-Thani kusema anaishangaa Saudi Arabia kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kauli iliyopingwa na Mfalme wa … Read More
Professa Muhongo amemuibua Kafulila Alikuwa Mbunge Kigoma Kusuni, David Kafulila ameibuka na kutoa kauli yake maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum kuhusiana na uchunguzi wa makontena 272 ya makinikia yaliyokuwa … Read More
Ratiba ya Sportpesa Super Cup Sport Pesa Cup 5/6 Singida united Vs FC leopardYanga Vs Tusker fc6/5 Simba Vs Nakuru All StarJang`ombe boys vs Gor mahiaNusu fainali tarehe 8Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya… Read More
Nikki wa Pili ampongeza Rais Magufuli Msanii wa Nikki wa Pili, amempongeza Rais Magufuli kwa kitendo alichokifanya leo cha kumtumbua Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo na kumwambia Mungu amsimamie katika kupambana na ufisadi.Niki ameto… Read More
0 comments:
Post a Comment