Mamia ya watu wameugua na mtoto mmoja amepoteza maisha kwa kile kinachoelezwa kutokana na kula chakula chenye vijidudu vyenye kusababisha magonjwa walipokuwa kwenye kambi karibu na mji wa Mosul.
Watu wamedaiwa kutapika na kuhara baada ya mlo wa futari baada ya mfungo wa Ramadhani.
Kambi ya Hasansham U2, kati ya mji wa Mosul na Irbil, huwapatia watu hifadhi wakitokea Iraq wakikimbia wapiganaji wa IS.
Wapiganaji wa IS wako mbioni kuzunguka magharibi mwa mji wa Mosul.
Shirika linalohudumia wakimbizi, UNHCR limesema kuwa visa takriban 800 vya maradhi vimerekodiwa huku watu wengine 200 wakipelekwa hospitali.
Kambi hiyo ni moja kati ya 13 zilizojengwa na UNHCR katika eneo la Mosul kwa ajili ya kuwatunza watu wanaokimbia kutoka mjini na maeneo ya vijiji.
Kambi hiyo inatunza watu 6235.
Vikosi vya Iraq, vikiungwa mkono na vikosi vinavyoongozwa na majeshi ya Marekani walianza Operesheni ya kuuchukua mji wa Mosul kutoka kwa wapiganaji wa IS mwezi Oktoba mwaka jana.
source:bbc
0 comments:
Post a Comment