Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya ametoa salamu kwa Wabunge wa CCM pamoja na Spika Job Ndugai kutambua kwamba hata baada ya kumuadhibu kutohudhuria vikao bya bunge siyo silaha ya kuwafunga midomo.
Bulaya amefunguka hayo akiwa Mkoani Kilimanjaro na kusema kwamba uamuzi uliofanya na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Wabunge CCM pamoja na Spika wa bunge haujawatendea haki wananchi wao kwa sababu ni kwa muda mrefu watakosa wawakilishi bungeni ingawa siyo mwisho kwa wao kupigania haki na kuwatumikia wananchi kwa njia zingine.
"Wamekosea sana kwa sababu wananyima wananchi wetu haki ya kupata wawakilishi wa matatizo yao bungeni. Ingawa tayari tumekwishaweza kujipanga namna ya kwenda kuwatumikia na kupeleka maendeleo kwa katika kipindi hichi ambacho tutakuwa nje ya bunge. Lakini niweke wazi adhabu hii kutolewa siyo silaha ya kutuifanya kuacha kupigania demokrasia na haki. Bulaya alifunguka.
Aidha Bulaya ametupa lawama kwa Mh. Ndugai na kudai kuwa ni kiongozi asiyeweza kuzuia hasira ndio maana amekuwa na maamuzi ya kuhukumu haraka wakati yeye ni baba anayepaswa kuwa na subira na uvumilivu wa kuongoza.
Mbunge Bunda Mjini, Mh. Esther Bulaya pamoja na Halima Mdeewa Kawe wamesimamishwa kuhudhuria vikao vyote vya Bunge vinavyoendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 kwa kile kinachodaiwa kuonyesha utomvu wa nidhamu ndani ya bunge.
source:muungwana
0 comments:
Post a Comment