Mwimbaji staa wa Bongofleva kutoka WCB Diamond Platnumz amefunguka kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM na kusema kuwa sifa ya kwanza ya WCB ni kumtoa msanii kwenye hali ngumu ili waweze kufanikiwa wote kwa kuwa huwa na adabu na kujituma.
Diamond amesema kuwa wengi wanaotoka katika familia a kitajiri wanakuwa hawana adabu kwa kuwa wanajua kwao kuna hela hivyo hawawezi kujituma ndiyo sababu WCB huchukua watu kutoka familia za chini ili wawashike mkono na wao waweze kusaidia ndugu zao.
“Kweli sifa ya kwanza WCB ni kutoa msanii ambaye ametoka kwenye familia ya chini – kwenye hali ngumu na maisha magumu kwa sababu sisi tunajitahidi kujiajiri wenyewe kwa wenyewe kutengeneza riziki japo muziki wetu haujawahi kuwa na riziki. Hivyo at list kidogo hiki tule wote.
“Kwa sababu tunaamini watu kutoka mtaani wanakuwa na vipaji vya kweli. Wanakuwa na njaa ya kujituma, wanakuwa na nidhamu na wanaogopa wasije kurudi tena katika mtaa lakini watoto wa kitajiri wanakuwa hawana nidhamu kwa kuwa wanajua kwao wana hela. Kwa hiyo, yeye haogopi kufanya kazi kwa bidii anajua hata asipofanya hivyo baba yake ana hela, akifa atarithi mali zake zote.
“Kwa hiyo, sisi tunaamini sana kwamba, wale wameshafanikiwa. Ni mara kumi sisi tukatumia nafasi hii kusaidia ndugu zetu wa mtaani kwa sababu wapo wengi wanaohitaji sisi tuwashike mkono nao wafike sehemu fulani. Kesho na kesho kutwa waje kuwasaidia ndugu zao.” – Diamond
Wednesday, 7 June 2017
Home »
» Diamond Platnumz ataja moja ya vigezo vya kujiunga na familia ya WCB
Diamond Platnumz ataja moja ya vigezo vya kujiunga na familia ya WCB
Related Posts:
Mpenzi wa jinsia moja achaguliwa waziri mkuu SerbiaHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionAna Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic. Rais wa Serbia amemteua mwanamke ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa waziri mkuu katika jimbo la kihafidhana la Balkan. Ana B… Read More
Waziri wa Tamisemi atoa onyo hili kwa wakuu wa mikoa na wilaya Dodoma. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia vibaya madaraka yao ya kukamata watu walio kwenye himaya zao.Ametoa onyo hilo leo (Ijumaa) … Read More
Kikwete uso kwa uso na Kardinali Pengo Dubai Dar es Salaam. Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo.Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo a… Read More
Mvutano waibuka baina ya CCM, ACT- Wazalendo kuhusu katiba mp Kutokana na mambo mbalimbali ambayo yanaendelea nchini ikiwepo mikataba mibovu ya madini viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamekuwa wakisema njia pekee ya kuweza kusaidia nchi kulinda maliasili zake ni kuwa na Katiba m… Read More
Uhamiaji imekamata mitambo ya kughushi nyaraka Kamishna wa Usimamizi wa Mipaka, Samwel Magweiga IDARA ya Uhamiaji imekamata mitambo ya kughushi nyaraka mbalimbali za idara hiyo pamoja na mashine za kielektroniki (EFDs).Akizungumza na waandishi wa habari jijini … Read More
0 comments:
Post a Comment