Timu za England na Venezuela zimetinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20.
England wametinga katika hatua ya fainali kwa kuichapa Italia kwa mabao 3-1 magoli ya England yamefugwa na Dominic Solanke aliyefunga mara mbili na Ademola Lookman huku goli pekee la Italia likifungwa na Riccardo Orsolini.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali Venezuela wamewachapa Uruguay kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya sare ya goli 1-1 katika dakika tisini za kwaida.
Mchezo wa fainali kati ya England na Venezuela utachezwa june 11 katika dimba la Suwon mchezo huo ukitanguliwa na mchezo wa mshindi wa tatu kati ya Italia na Uruguay.
0 comments:
Post a Comment