Thursday, 8 June 2017

Dkt Mpango awasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2016

Responsive image
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2016 na Mpango wa maendeleo ya uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2017/2018.

Akiwasilisha taarifa na mpango huo bungeni mjini Dodoma, Waziri Mpango ametaja vipaumbele kuwa ni  ujenzi wa miundombinu, kuimarisha vyanzo vya mapato, kuboresha huduma za jamii, mazingira ya viwanda na upatikanaji wa nishati.

Waziri Mpango amesema uchumi wa taifa umeongezeka kwa asilimia Tano huku hali ya umaskini hususani vijini imepungua kwa asilimia moja.

0 comments:

Post a Comment