Tuesday, 13 June 2017

Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi Kenya


Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Image captionJumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Karibu watu 15 hawajulikani waliko baada ya jumba la ghorofa saba kuporomoka usiku wa kuamkia Jumanne, katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, liliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa makundi ya uokoaji yako eneo la mkasa katika kijiji cha Kware Pipeline mtaa wa Embakasi.
Gazeti la Star nchini Kenya lilisema kuwa watu kadha waliokolewa kabla ya jumba hilo kuporomoka.
Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Image captionJumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Walioshuhudia waliliambia gazeti hilo kuwa jumba hilo lilikuwa limeonyesha dalili baada ya nyufa kuonekana kwenye kuta zake.
Mratibu wa shughuli za uokoaji Pius Masai anasema kuwa zaidi ya watu 100 wanatambulia kuwa salama lakini akaongeza kuwa huenda watu wengi wamekwama.
Idara inayoshughulikia majanga inasema kuwa familia nyingi ziliondoka wakati ziliamriihwa kabla ya jengo hilo halijaporomoka ambapo watu 121 waliondoka salama.
Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Image captionJumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Vyombo vya habari vinasema kuwa baadhi ya watu walirudi tena ndani jengo hilo kuchukua mali yao wakatai liliporomoka.
Polisi wanasema kuwa hawafahamu ni watu wangapi ambao wamekwama ndani ya jengo lililopomoka.
Jumla ya watu 49 walifariki wakati jumba lingine liliporomoka kufuatia mvua kubwa mwezi Aprili mwaka huu.
Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi
Image captionJumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi

Related Posts:

  • Trump 'atengwa' na wenzake G7Image captionRais Trump ametengwa na wenzake kuhusiana na makubaliano ya tabia nchi yaliofakiwa mjini Paris Viongozi katika mkutano wa G7 wametofautiana kuhusu taarifa ya mabadiliko ya tabia nchi. Viongozi sita walikubaliana… Read More
  • Wauawa kwa kuwalinda wanawake Waislamu MarekaniHaki miliki ya pichaCBS/EVNImage captionPolisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati Polisi katika mji wa Portland nchini Marekani, wanasema wanaume wawili waliuawa, walipo… Read More
  • Gavana asema al-Shabab huenda wakateka eneo la KenyaImage captionRamani ya Somalia Viongozi wa eneo la mashariki nchini Kenya wameonya kwamba maeneo ya taifa hilo huenda yakanyakuliwa na wapiganaji wa Al-Shabab. Gavana wa kaunti ya Wajir ambayo inapakana na taifa la Somalia a… Read More
  • Marekani kufanya majaribio ya kudungua komboraImage captionMfumo wa kudungua makombora wa Marekani uliopelekwa Korea Kusini Idara ya jeshi nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi … Read More
  • Bomba la kupitisha pombe kujengwa UjerumaniHaki miliki ya pichaAFPImage captionPombe itakuwepo kwa wingi katika tamasha hilo Waandalizi wa Tamasha maarufu la muziki wa rock nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja zaidi ya elfu 75 kwamba, katu! hawatokumbwa na kiu ya … Read More

0 comments:

Post a Comment