WATUNGA sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka.
Mchumi wa nchi hiyo, Gus Faucher, anasema ni hali ya kushangaa kuonekana Dola za Marekani, inashuka thamani hivi sasa.
"Nadhani takwimu tulizopata kutoka mkutanoni inaonyesha vigezo," anasema Faucher, huku wachumi wakieleza shaka yao dhidi ya hali halisi ya sera za Rais mpya, Donald Trump.
Inaelezwa kwamba katika kipindi kifupi kilichopita, tangu Machi mwaka huu, serikali iliongeza kiwango cha riba zake mara tatu.
Pia, katika sura nyingine, inaelezwa kuwa benki zimeendelea kuwa imara katika majukumu yake ya kila siku.
Kwa miaka mingi na katika sehemu nyingi, Dola ya Marekani imekuwa marejeo cha kiwango cha mabadilishano katika fedha za dunia.
Pia, kuna fedha kama za Euro ambazo ni za Jumuiya ya Ulaya (EU) na Pauni za Uingereza, nazo zimeshika nafasi hiyo .
0 comments:
Post a Comment