Thursday, 25 May 2017

Mauaji Pwani yamepangwa: Mbunge

Dodoma. Mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji jana yaliibuka bungeni kwa mara ya pili, wakati mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa alipoeleza siri ya mipango na kiini chake.

“Nataka niseme na Rais wangu ajue. Mambo haya yanayotokea, hayatokei kwa bahati mbaya. Mambo haya yana root cause (kiini chake). Mambo haya yamepangwa,” alisema mbunge huyo na kuongeza:

“Yapo mambo mengi, zipo chuki nyingi zimejengwa kwa wananchi. Yapo mambo mengi yalifanyika yanatoa kero kubwa kwa wananchi ndio maana gazeti la leo (Mwananchi) lilipoandika taarifa hizi, mimi sikushangaa kwa sababu ninajua yako hayo mambo.”

Mbunge huyo alisema yako mambo Serikali inapaswa kuyafanya na iwe sasa kwa sababu jambo hilo ni kubwa, linaendelea kutanuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

  Mchengerwa alitoa kauli hiyo jana baada ya Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini kuomba mwongozo kwa kutumia kanuni ya 47(1), akitaka Bunge liachane na shughuli za mezani na kujadili usalama katika maeneo hayo.

Mbunge huyo alisema Waziri Mwigulu alipotembelea maeneo hayo alitoa maagizo mazuri, lakini yametafsiriwa vibaya na polisi ambao wanakamata na kupiga watu hovyo.

“Hivi karibuni walimkamata Sultani Mpiji aliyekuwa akifua nguo. Baba yake amekuta maiti yake Muhimbili. Wananchi wanalalamika, wananchi wanahamahama, hali si nzuri. Hali ni mbaya sana,” alisema.

source:muungwana

Related Posts:

  • Ole Sendeka atuma salamu hizi kwa Lowassa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Ac… Read More
  • Simba yatumia Mil. 100/ kumshawishi Niyonzima NI UMAFIA TU! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya Sh. milioni 100. Habari zilizopatikana jana jioni … Read More
  • Nchemba amtolea uvivu Tundu Lissu  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ‘amemvaa’ Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kwamba amejaribu kutengeneza kila aina ya kichaka kukwamisha jitihada za Rais John Magufuli kupambana na usafirish… Read More
  • Hoja 6 moto mkali kwa serikali bungeni MJADALA wa mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 unatarajiwa kuhitimishwa leo mjini hapa huku hoja sita zikionekana kuwa mtihani mgumu kwa serikali kuzitolea majibu kesho wakati in… Read More
  • Vigogo wawili Waliotajwa Ripoti ya Makinikia wamwaga fedha Kanisani WABUNGE watatu, wakiwamo Andrew Chenge na William Ngeleja ambao Kamati ya pili ya Rais kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusiana na makinikia Jumatatu iliyopita ilishauri wachunguzwe, jana walitoa mchango kwa k… Read More

0 comments:

Post a Comment