Tuesday, 30 May 2017

Vifaru vya Urusi vinavyotia wasiwasi mataifa ya Nato barani Ulaya

Armata tank in Red Square, Moscow, 9 May 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionArmata ni kifaru cha kisasa ambacho kinachukua nafasi ya vifaru vya enzi za muungano wa Usovieti
Urusi imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya mfumo wake wa kukabiliana na vifaru wakati wa vita.
Vifaru hiyo vipya vya Urusi kwa jina Armata T-14 vinaundwa vikiwa na teknolojia ya Kinga Dhidi ya Makombora (APS).
Lengo la teknolojia hiyo ni kuwezesha vifaru hivyo kutoharibiwa na makombora mengi yaliyoundwa kukabiliana na vifaru, yakiwemo yale aina ya Javelin yanayoundwa Marekani, ambayo yanatumiwa na jeshi la Norway.
Brigidia Ben Barry wa taasisi kuhusu usalama wa kimataifa ya International Institute for Strategic Studies (IISS) mjini London anasema mataifa yanfaa kuanza kufikiria upya teknolojia yake ya kukabiliana na makombora.
Anasema mataifa mengi ya Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi (Nato) hayajagundua tatizo linalowakabili.
Teknolojia ya APS inatishia kufanya silaha nyingi za kukabiliana na vifaru kutofanikiwa, na mataifa mengi ya Magharibi hayajaanza kujadiliana kuhusu hatua za kuchukua.
Anasema baadhi ya nchi zinafanya utafiti na majaribio kivyake kuweka mfumo huo wa APSkwenye vifaru vya mataifa hayo.
"Lakini yanakosa kuzingatia matokeo ya teknolojia hii kwa mfumo wao wa kukabiliana na vifaru,2 anasema.
Norway ni moja ya nchi za kwanza kukumbana na hatari hii.
Nchi hiyo inapanga kutumia krona 200-350m (£18.5-32.5m; $24-42m) kubadilisha makombora yake ya Javelin na "kudumisha uwezo wake wa kukabiliana na vifaru".
"Kuna haja ya kuwa na makombora ambayo yanaweza kupenga mfumo wa APS."
APS
  1. Adui anarusha kombora au mzinga kushambulia kifaru
  2. Mfumo kwenye kifaru unagundua kuna tishio njiani
  3. Teknolojia ya rada inahesabu njia na pahali palipolengwa
  4. APS inarusha kombora la kuharibu kombora au mzinga
  5. Kombora au mzinga wa adui unaharibiwa
Teknolojia ya APS imebadilisha mambo katika historia ya kuangazia kushambulia na kujilinda wakati wa vita.
Katika vipindi fulani, kuna moja ambayo ilikuwa mbele.
Zamani, vifaru visivyoweza kupenya risasi vilitawala, lakini makombora nayo yakaimarisha na kumaliza ubabe huo.
Tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, vifaru vimeendelea kutawala katika uwanja wa vita.
Vifaru hata hivyo, huwa vinaweza kuharibiwa na makombora au mabomu ya vifaru vingine vikiwa karibu.
Lakini kulikuwa pia na tishio kutoka kwa silaha nyingine, mfano makombora ya kurushwa kutoka mbali au kutoka kwa ndefe, jambo ambalo ndilo teknolojia ya APS imeundwa kukabili.
Infographic of Armata T14 tank
Anti-tank training in South Korea, 2006Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMakombora ya kurushwa kwa kutumia mizinga ya kubeba mabegani yanaweza kuharibu makombora. Hapa, ni mazoezi ya kukabili makombora Korea Kusini, mshirika wa Marekani.
Israeli Merkava tank, 2014Haki miliki ya pichaAFP
Image captionVifaru vya Israel aina ya Merkava huwa na teknolojia ya APS
Israel ni miongoni mwa mataifa ambayo yamekuwa yakiongoza katika teknolojia ya kujikinga na vifaru vyake aina ya Merkava hutumia teknolojia hii.
Vifaru hivyo vilitumiwa kukabiliana na wapiganaji wa Kipalestina ukanda wa Gaza.
Mfumo huo wa Israel pia unachunguzwa na Wamarekani.
Uingereza pia imeanza kutafakari uwezekano wa kustawisha teknolojia kama hiyo.
Uholanzi imeamua kutumia teknolojia nyingine, pia kutoka Israel, kukinga vifaru vyake.

source:bbc

Related Posts:

  • Mtaji wa Soko la Hisa DSM waporomoka Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) umepungua kwa Shilingi Bilioni 380 kutoka Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.9 kwa wiki iliyoishia Mei 19 mw… Read More
  • Nape amemjibu Makonda, Picha limeanza upyaaa Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhojiwa na kituo cha Star Tv kuhusu mambo kadha wa kadha likiwemo suala la uvamizi wa Clouds Media na kusema Hakupaswa kumuingilia kwakuwa wote ni watumishi... Basi Nape ame… Read More
  • Mbunge atinga bungeni na rundo la risiti Dodoma.Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Rhoda Kunchela aliwasilisha bungeni furushi la risiti za mwenge wanazodaiwa kuchangishwa kwa nguvu, walimu na wafanyabiashara.Mbunge Kunchela aliomba kutoa hoja ili ijadiliwa na Bunge … Read More
  • Nyumba zateketea kwa moto Sengerema Sengerema. Nyumba za wavuvi ambazo idadi yake haijajulikana hadi sasa katika kisiwa cha uvuvi cha Nyamango Kata ya Bulyaheke  halmashauri ya Buchosa wilayani hapa, zinateketea kwa moto ambapo chanzo chake hakijajul… Read More
  • Polisi watangaza dau la Mil. 60 Ukiwakamatisha hawa JESHI la Polisi mkoa wa Pwani limetangaza zawadi ya Sh. milioni tano kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mku… Read More

0 comments:

Post a Comment