Tuesday 30 May 2017

Wafanya biashara jijini Mwanza watishia kufanya mgomo Juni tano mwaka huu

Maelfu ya wafanyabiashara wa Soko kuu la Jijini Mwanza, Mlango mmoja pamoja na Buzuruga, Juni 5 mwaka huu wametishia kufanya mgomo usiokuwa na kikomo yakiwemo maandamano, kwa lengo la kupinga upandishwaji wa gharama za kodi ya pango la biashara bila kushirikishwa.

Baada ya halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, kupandisha kodi ya pango kutoka shilingi 50,000 hadi 4000,000/=, wafanyabiashara hao wanaangua vilio, ili Serikali iweze kuwasikiliza

Kilio cha wafanyabiashara hao kimetolewa mbele ya waandishi wa habari katika eneo la soko kuu la Mwanza, baada ya baadhi yao kusitisha shughuli za kujitafutia kipato, kutokana na uzito wa ongezeko la kodi hiyo.

Kutokana na kilio hicho Ofisi ya Rais, tawala za mikoa na Serikali za mitaa kupitia barua yenye kumbukumbu No. CB 78/237/01 ya Machi 10 mwaka huu, tayari imeshaiagiza Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kushughulikia hoja hizo.

Kwa mantiki hiyo Channel, ikalazimika kuwatafuta wakurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kuzungumzia suala hilo, ambapo baada ya kupatikana wakasema kuwa msimamo wa kodi hizo hautabadilishwa na atakayeshindwa kulipa aachie eneo.

0 comments:

Post a Comment