Tuesday 30 May 2017

Upepo mkali watarajiwa kuvuma pwani ya Tanzania

Mtumbwi
Image captionWanaotumia bahari wametakiwa kuchukua tahadhari Tanzania
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania.
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka hiyo, kupitia taarifa, imesema kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2.
"Msukumo wa upepo wa Kusi unatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania," mamlaka hiyo ilisema.
"Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki."
Hali hiyo ya hewa inatarajiwa kuwepo hadi kufikia kesho 31 Mei.

0 comments:

Post a Comment