Sunday, 28 May 2017

Polepole aonywa kauli yake ya Mauaji Kibiti


Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi.
Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani Morogoro akitokea Dar-s-Salaam.

Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya.

Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa.

“Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na wala siyo kipindi muafaka wakati taifa lina majonzi makubwa,"alisema.

Related Posts:

  • BAADA YA KIFO:ndugu wataka uchunguzi kifo cha Ndesamburo Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemone Ndesamburo amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya KCMC, Mkoani humo.Katib… Read More
  • Rais Magufuli amlilia Mwasisi wa Chadema Rais John Magufuli amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha  mmoja wa waasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Phillemon Ndesamburo huku akimtaja marehemu kuwa alikuwa kiongozi mwenye hekima na aliyez… Read More
  • Mbunifu wa Android azindua simu mpya ya EssentialHaki miliki ya pichaESSENTIAL PHONEImage captionSinu ya Essential hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699. Andy Rubin, ambaye ni miongoni mwa watu waliobuni programu ya software Android ya Goo… Read More
  • Ndugai amkumbuka kwa majonzi Ndesamburo Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anamkumbuka marehemu Phillemon  Ndesamburo aliyekuwa mbunge wa Moshi  Mjini (Chadema) kwa uchapakazi wake na mapenzi yake makubwa kwa wapiga kura wake.“Nimepokea kwa masikitiko t… Read More
  • Kambi ya Upinzani Bungeni uvunjwe MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), amelitaka Bunge kuvunja Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na maoni ya kambi hiyo kutosikilizwa.Lema amedai kuna kuchujwa kwa maneno yanayochangiwa na wabunge w… Read More

0 comments:

Post a Comment