Monday, 29 May 2017

Mgombea urais adaiwa kutaka kujirusha kutoka kwenye ghorofa Kenya

Baadhi ya wanaume wakisajiliwa kama wapiga kura nchini Kenya kufuatia kuanzishwa kwa shughuli hiyo siku ya Jumatatu
Image captionRaia wakijisajili kuwa wapiga kura nchini Kenya awali. Uchaguzi mkuu utafanyika Agosti 8
Mmoja wa waliojitokeza kugombea urais katika uchaguzi mkuu mwezi Agosti nchini Kenya alijaribu kujirusha kutoka jumba la ghorofa, taarifa katika vyombo vya habari nchini humo zinasema.
Bw Peter Solomon Gichira anadaiwa kujaribu kujirusha kutoka ghorofa ya sita katika afisi za Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) jijini Nairobi baada ya ombi lake la kutaka kuwania urais kukataliwa Jumamosi jioni.
Mkuu wa polisi wa Nairobi Japheth Koome amesema Bw Gichira atafunguliwa mashtaka ya kuzua fujo eneo la umma, kuharibu mali na kujaribu kujitoa uhai.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, mkuu wa polisi wa kituo cha Central Robinson Thuku alisema Bw Gichira alikuwa ameenda afisi za IEBC kufuatilia ombi lake alipofahamishwa kwamba ombi lake lilikataliwa.
Ni hapo ambapo alianza kulalamika na akavunja dirisha na kujaribu kuruka nje lakini akazuiwa na maafisa wawili ambao pia walimkamata.
Bw Thuku alisema mwanasiasa huyo atafikishwa mahakamani Jumatatu.
Polisi walikataa kumwachilia dhamana na kusema wanamzuilia kwa ajili ya usalama wake.
Mgombea mwenza wa Bw Gichira, Kelly Watima, hata hivyo alisema mwenzake amekuwa akihangaishwa tangu alipotangaza nia ya kutaka kuwania urais.
"Bw Gichira amekuwa akihangaishwa na maafisa wa IEBC na sasa polisi wanamzuilia ndipo akose fursa ya kuwasilisha karatasi zake za uteusi …mbona wanamuogopa…je, ni kwa sababu ni tishio kwao?" alisema, kwa mujibu wa Daily Nation.
Bw Gichira ni miongoni mwa wanasiasa kumi waliokuwa wameeleza nia ya kutaka kuwania urais lakini wakakosa kuidhinishwa na tume hiyo kwa kukosa kutimiza amsharti mbalimbali.
Kuna wagombea kumi walioidhinishwa, ambao wamekuwa wakiwasilisha karatasi zao Jumapili na leo Jumatatu.
Miongoni mwa waliofanikiwa kuwasilisha karatasi zao Jumapili ni aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, mgombea huru Ekuru Aukot na Abdouba Dida ambaye pia aliwania urais mwaka 2013.
Waliopangiwa kuwasilisha karatasi zao za uteuzi leo ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta ambaye anawania kwa mara ya pili.


source:bbc

Related Posts:

  • Irene Uwoya ateuliwa kuwa balozi KAMPUNI ya simu za mkononi ya itel mobile Tanzania leo imetiliana saini na msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya kuwa balozi wake atakayeitangaza kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Akizungumza katika hafla hiyo Haf… Read More
  • Taarifa Muhimu kutoka Idara ya Elimu Chalinze Mkoani Pwani IDARA ya elimu Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeishukuru Serikali Kuu kwa kuwapatia vitabu 109, 673 vyenye thamani ya zaidi ya sh. Mil. 117. Afisa elimu Halmashauri hiyo Bi. Zainabu Makwinya… Read More
  • Mzee Yusuph anakutaka ufute nyimbo zake kwenye simu yako Aliyekuwa mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amefunguka na kueleza kuwa watu wote walio na nyimbo zake kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi. Katika mahojihano na kipindi cha Mitikis… Read More
  • Adhabu kali kwa Raia Wanaoishi bila ndoa Burundi Pierre-Nkurunziza Rais wa Burundi Watu wanaoishi katika mahusiano ya mume na mke bila kufunga ndoa nchini Burundi wameamrishwa kwamba wawe wameoana rasmi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu la sivyo wataaadhibiwa vikali. Ms… Read More
  • Naibiwa sana Wanaume- Wolper Muigizaji Jacquline Wolper amekanusha vikali kuhusu suala la kuwahi kubadilisha dini kwa shinikizo la mapenzi na kwamba yote yaliyowahi kuonekana au kusikika huko nyuma ni mambo ya sanaa. Jacqueline Wolper anadai kuwa m… Read More

0 comments:

Post a Comment