Thursday 25 May 2017

Mbunifu wa Nembo ya Taifa ahamishiwa Hosptali ya Muhimbili


Mzee Francis Ngosha ndiye mchoraji na mbunifu wa nembo ya taifa maarufu kama Bibi na Bwana, S iku mbili zilizopita aliliripotiwa kuwa anaishi maisha ya Magumu huko Buguruni jijini Dar es salaam. Kibanda alichokuwa akiishi ni cha hovyo sana mithili ya  banda la kuku limezungushwa na Bati juu mpaka chini.

Baada ya taarifa hiyo kutolewa na vyombo vya habari, Serikali imesema kuanzia sasa itaanza kumpatia huduma za matibabu na kijamii Mzee Francis Ngosha, mbunifu wa Nembo ya Taifa ya bibi na Bwana.

Ambapo Mzee Ngosha amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akitokea Amana alikokuwa amelazwa tangu jana (Jumatano).

Ngosha amehamishwa hospitalini hapo baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla kumtembelea leo asubuhi kumjulia hali.

Katika mazungumzo, Ngosha amesema alichora nembo hiyo akiwa na mwenzake Ali Pangani ambaye amefariki dunia.

"Nimetumwa nije kumuona mzee wetu aliyechora nembo ambayo ni utambulisho wa Mtanzania, tumemuhamisha hapa na kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi," anasema Dk Kigwangalla.
source:muungwana

0 comments:

Post a Comment