Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz ameandika ujumbe huu "Mbele yako, Nyuma yetu" Ujumbe huo ni baada ya Aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’, Ivan Semwanga kufariki dunia akiwa hospitali nchini Uganda alipokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo usiku wa kuamkia leo Mei 25, 2017.
Ivan aliyekuwa baba wa watoto watatu wa kiume wa Zari, aliachana na mwanamama huyo miaka michache iliyopita ambapo Zari alihamishia mapenzi kwa mwanamuziki Diamond Platinumz ambaye mpaka sasa wamezaa watoto wawili, wa kike mmoja na wa kiume mmoja.
Ivan alikuwa maarufu Afrika Mashariki kutokana na biashara zake kubwa alizokuwa akifanya zikiwemo umiliki wa vyuo mbali mbali nchini Afrika Kusini, pamoja na Tycoon Ivan.
0 comments:
Post a Comment