Hospitali ya Mercy ya Marekani, imebainisha kuwa huenda watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent wakaruhusiwa kutoka hospitali wakati wowote kuanzia kesho.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika leo, Alhamisi kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa huenda watoto Sadia Ismael na Wilson Tarimo wakaruhusiwa.
“Hali za watoto hawa wawili zimesemekana kuimarika kuruhusu wapelekwe kwenye kituo maalumu kwa uangalizi wa karibu na kufanyiwa mazoezi ya viungo ambako wataendelea kukaa na kuhudumiwa.”
“Mtoto Doreen ataendelea kuwepo hospitali katika wodi ya watoto akiendelea kupata huduma za karibu hadi itakapoamuliwa vinginevyo,”ameandika Nyalandu.
source:muungwana
Thursday, 25 May 2017
Home »
» Nyalandu: Majeruhi wa Lucky Vicent kuruhusiwa Hospotali kesho
0 comments:
Post a Comment