Mimba imekuwa ni chanzo kimojawapo kinachochangia kurudisha nyuma ustawi wa elimu hapa nchini.
Wanafunzi 33 wa sekondari wilayani Meatu mkoani Simiyu wamekatisha masomo yao baada ya kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka 2016 hadi mwezi April mwaka huu.
Afisa Elimu sekondari wilaya ya Meatu, Estomih Makyara ametoa takwimu hizo katika kikao cha baraza la madiwani baada ya hoja kutolewa na baadhi ya madiwani wakimtuhumu mwalimu wa shule ya sekondari kumpa ujauzito mwanafunzi.
madiwani wameshauri uwepo wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike huku wakisisitiza kuchukuliwa kwa hatua kali kwa watakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment