Friday, 26 May 2017

Mji wa Marawi nchini Ufilipino wavamiwa na IS

Sheria ya kijeshi iliwekwa kwenye kisiwa cha Mindanao kutokana na machafuko mjini MarawiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSheria ya kijeshi iliwekwa kwenye kisiwa cha Mindanao kutokana na machafuko mjini Marawi
Serikali ya Ufilipino imesema mji ambao upo kusini mwa kisiwa cha Mindanao umevamiwa na wapiginaji wa kundi la Islamic state.
Kwa zaidi ya siku mbili,Wanajeshi wa nchi hiyo wamekua wakitekeleza mashambulizi ya anga katika mji wa marawi,ambao umevamiwa na wanamgambo wa IS. Mapambano hayo yalianza baada ya wanajeshi wa Serikali kuvamia nyumba moja ikimtafuta Isnilon Hapilon, Kiongozi wa IS nchini Ufilipino na kiongozi wa kundi la Abu Sayyaf.
Wanamgambo waliungana na wapiganaji kutoka Malaysia na Indonesia na wamewashika mateka takriban watu 11 kutoka kanisa katoliki.
Takriban wanajeshi na Polisi 40 wameuawa kwenye mapambano ya kurushiana risasi, ambayo yamesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.

Related Posts:

  • Kikwete aanza kazi na Mgogoro wa Libya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho kikwete ameanza kazi kama Mwenyekiti Mwenza katika Baraza la Kimatifa la Wakimbizi ambapo ameanza kazi yeye na jopo lake ya kutaka kusuluhisha Mgororo wa muda mrefu wa nchin ya Libya. Kikwete … Read More
  • Kashfa nzito zaikumba Wizara ya maliasili BAADHI ya wabunge wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii, kukamata na kupiga mnada mifugo inayoingia kwenye hifadhi za taifa. Kutokana na vitendo hivyo, watunga sheria hao wameishauri serik… Read More
  • Wajumbe wa kamati Iliyomng'oa Muhongo walitishwa RAIS Dk. John Magufuli amebainisha kuwa licha ya kamati ya Kuchunguza Makontena ya Mchanga wenye Madini (makinikia) kupewa ulinzi mkali, kulikuwapo vitisho na hata baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa. Akizungumza jana wak… Read More
  • Mauaji Pwani yamepangwa: Mbunge Dodoma. Mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji jana yaliibuka bungeni kwa mara ya pili, wakati mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa alipoeleza siri ya mipango na kiini chake.“Nataka niseme na Rais wangu ajue. Mambo … Read More
  • Msanii aliyebuni nembo ya Taifa sakata lake latua bungeni Dodoma. Bunge jana lilielezwa kuwa msanii aliyebuni na kutengeneza nembo ya taifa ya Bibi na Bwana, Francis Ngosha ametelekezwa na taifa na anaishi maisha magumu.Suala la msanii huyo liliibuka Bungeni mjini Dodoma leo, kuto… Read More

0 comments:

Post a Comment