Friday, 26 May 2017

Kenya: Afariki dunia baada ya kutabiri kifo chake


 Irene Chris aliolewa kwa harusi Agosti 2016 na mumewe Chris Mwangi - Mnamo January 2017,

Irene aliandika katika mtandao wa kijamii kwamba alikuwa akielekea mbinguni na kuwaomba watu kutuma salamu -Miezi minne baadaye, mwanamke huyo mrembo ameaga dunia na marafiki wake wamejua kuwa alikuwa na hisia kwamba angeaga dunia

Irene Chris, mkewe Chris Mwangi alikuwa na maono ya kifo chake. Alidokeza hata katika mitandao ya kijamii ingawa ni wachache waliofahamu.

Harusi ya Irene ilikuwa Agosti 2016 na ilihudhuriwa na marafiki na familia yake. Katika ujumbe alioweka katika mtandao wa kijamii, miezi kadhaa baada ya kufanya harusi,

Irene aliwaomba marafiki wake kumtuma salamu kwa kusema kuwa alikuwa akielekea mbinguni.
Wengi marafiki wake walimkosoa kwa kusema hilo na kumwambia kuondoa ujumbe huo pamoja na kukoma kuzungumzia kifo.

Wengine walipizilia mbali ujumbe huo kwa kusema ulikuwa utani. Katika ujumbe mwingine, alisema alikuwa akikumbuka marafiki wake waliokufa. Lakini hakuna aliyeshikanisha jumbe hizo kwamba alikuwa akiwaaga kwaheri.

Irene alizikwa nyumbani mwa mumewe Wanyororo, Lanet, Kaunti ya Nakuru Alhamisi Mei 25 na kuacha mumewe na mtoto wake wa wiki mbili.

0 comments:

Post a Comment