Friday, 26 May 2017

Povu lamtoka Wolper kuhusu madai ya Kunuka Mwili

Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’.

Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’ ametokwa povu si la nchi hii baada ya kubanwa kuhusiana na madai ya kunuka mwili na kusema hajawahi kunuka maishani mwake na kwamba ingekuwa hivyo asingepapatikiwa na wanaume.

Hivi karibuni Ijumaa lilimfungia kazi msanii huyo nyumbani kwake na katika moja ya maswali aliyobanwa lilikuwa juu ya ishu iliyosambaa kuwa eti anatoa harufu mbaya sehemu za mwili wake.

Katika kuonesha kumaindi ile mbaya kuhusu madaia hayo, mrembo huyo ambaye kiukweli yuko bomba kwa muonekano alifunguka: “Aliyekuambia nanuka nani? Mimi sinuki wala sijawahi kunuka maishani mwangu, kuthibitisha hilo kwanza nisingekuwa napapatikiwa na wanaume kila kukicha sambamba na kuhongwa vitu kibao huku wengine nikiwaacha wakinililia.

Hao wanaosema na kusambaza hayo ni njia tu ya kujipatia followers kwenye mitandao yao kupitia mimi.” Wolper hakuishia hapo aliendelea kumwaga povu kuwa, tangu afungue duka la nguo ambalo amewekeza zaidi ya shilingi milioni 60, watu wengi wamekuwa wakichukizwa na maendeleo hayo. “Wana chuki tu na mimi, tangu nimefungua duka wananichokonoa, wanalishadadia hili jambo kisa tu nimepata mafanikio ya kufungua duka,” alipigilia msumari.

0 comments:

Post a Comment