Friday, 26 May 2017

Msichana aliyechomwa kwa tindi kali abahatika kupata mchumba India

Lalita Ben Bansi na mumewe Ravi ShankarHaki miliki ya pichaSHUTTERSTOCK
Image captionLalita Ben Bansi akivalia nguo yake ya harusi na mumewe Ravi Shankar
Muathiriwa wa shambulio la tindi kali India, Lalita Ben Bansi alicheka kwa furaha katika harusi yake mjini Mumbai wiki hii.
"Nani angedhani kwamba baada ya kuchomwa kwa tindi kali na kufanyiwa upasuaji mara 17 nitaweza kupata mpenzi? lakini limefanyika," ameliambia gazeti la Hindustan Times katika sherehe iliofanyika huko Thane.
Alifanikiwa kumpata mumewe baada ya kupiga simu nambari iliokoseka.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyeshambuliwa na jamaa yake mnamo 2012, amesema kufanikiwa kupata mpenzi ni kama miujiza.
"Bi Bansi alipiga simu yangu kwa bahati mbaya miezi mitatu iliyopita. Nilimpigia tena baada ya siku 15," Bwana Singh, mwenye umri wa miaka 27, anayefanya kazi na kampuni ya CCTV ameliambia gazeti la The Hindu.
"Tulizungumza na nikaipenda sauti yake. Tuliendelea kuzungumza kila siku na ni hapo ndipo nikamuomba kumuoa," alisema.
Wakati wa mazungumzo yao, Bi Bansi alimueleza Bwana Singh kwamba yeye ni muathiriwa wa shambulio hilo la tindi kali.
"Lakini nilimuambia kwamba ninampenda na ningependa kumuoa. Wachumba wengi hupendana kwa sababu ya sura na miwshowe huishia kutalakiana. Lakini kwake mimi sikuvutiwana sura, yeye ni mtu mzuri, naomba Mungu atubariki maisha yetu yote," aliongeza.
Harusi yao imehudhuriwa na nyota wa filamu za Bollywood akiwemo muigizaji Vivek Oberoi, aliyekutana na Bi Bansi katika hafla iliyoandaliwa kwa waathiriwa mashambulio ya tindi kali.
Nyota huyo alimtaja bi harusi kuwa "shujaa wa kweli". Alimsifu bwana harusi pia kwa kumpenda vile alivyo.
Inakadiriwa kwamba nchini India, kuna mashambulio 1,000 ya watu kumwagia tindi kali kila mwaka, licha ya kwamba inadhaniwa visa vingi haviripotiwi.

0 comments:

Post a Comment