Morogoro. Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi.
Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani Morogoro akitokea Dar-s-Salaam.
Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya.
Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa.
“Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na wala siyo kipindi muafaka wakati taifa lina majonzi makubwa,"alisema.
Sunday, 28 May 2017
Home »
» Mgeja akasirishwa na kauli ya Polepole
Mgeja akasirishwa na kauli ya Polepole
Related Posts:
Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya … Read More
Chelsea: Diego Costa amesema klabu hiyo inataka kumuuza Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionCosta amesema angependa sana kurejea Atletico Madrid Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa amesema amefahamishwa na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte kwamba hayupo tena katika… Read More
Shambulizi la bomu lasababisha vifo vya watoto wawili Nigeria Watoto wawili wameripotiwa kufariki huku watu wengine watatu wakiwa wamejeruhiwa baada ya shambulizi la bomu kutokea Nigeria.Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na polisi wa Adamawa ni kwamba mtu asiejulikana aliingia katika … Read More
Iringa: Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavangala kilichopo katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa na kupora fedha tasilimu kiasi cha zaidi ya shil… Read More
Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya … Read More
0 comments:
Post a Comment