Tuesday 23 May 2017

Maneno ya Kiswahili yaongezwa kamusi ya Kiingereza Kenya

Mwendeshaji pikipiki akiwa amembeba abiriaHaki miliki ya pichaAFP
Maneno kadha ya Kiswahili yameongezwa kwenye kamusi ya Kiingereza ambayo inakusudiwa kutumiwa na wanafunzi wa shule za msingi nchini Kenya.
Kamusi hiyo imechapishwa na matbaa ya Chuo Kikuu cha Oxford (OUP), na ni makala ya tatu.
Pia, kuna maneno yenye asili ya lugha nyingine za Afrika Mashariki au yaliyotoholewa na kuanza kutumiwa katika Kiswahili, ambayo yameongezwa kwenye kamusi hiyo.
Miongoni mwa maneno hayo ni:
Bodaboda - Baiskeli au pikipiki inayotumiwa kwa uchukuzi wa abiria
Mwananchi - Kwa maana ya mtu wa kawaida au raia wa kawaida
Daladala - (nchini Tanzania) mabasi madogo yanayotumiwa kwa uchukuzi wa abiria
Sambaza - Kugawa au kueneza kitu muhimu au cha thamani kwa watu wengine
Mwalimu - Neno linalotumiwa kabla ya kutaja jina la mtu anayeheshimika au anayeenziwa, ambaye anaweza kutoa ushauri au ujuzi kwa wengine. Mfano, Mwalimu Nyerere.
Mwanzilishi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage NyerereHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMwanzilishi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Maneno ya Kiswahili ambayo yamewahi kuingizwa kwenye kamusi za Kiingereza ni pamoja na Shamba na Safari. 
Hii ni dalili nzuri sana kwa lugha ya kiswahil hasa katika nchi ya tanzania.

0 comments:

Post a Comment