Tuesday, 23 May 2017

Sylvester Stallone aridhia filamu ya Rambo iigwe Bollywood

Sylvester StalloneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSylvester Stallone ametuma ujumbe kuunga mkono kuigwa upya filamu hiyo kihindi
Kupokea ujumbe kutoka kwa Sylvester Stallone kuhusu kuigwa upya filamu ya Rambo kihindi ni kama "kuungwa mkono na Mungu", mkurugenzi wa filamu hiyo amesema.
Sid Anand ameambia mashabiki filamu hiyo haitokuwa na nyimbo na kucheza dansi kama ilivyozoeleka kwa filamu za Bollywood .
"Siwezi kuifanya hivyo Rambo," ameimbia BBC. "Itakuwa ni kama kumkosea Mungu."
Filamu hiyo inazinduliwa katika maonyesho ya filamu ya Cannes .Hata hivyo filamu yenyewe itaanza kurekodiwa baadaye mwaka huu.
Shroff na picha ya RamboHaki miliki ya pichaRAMBO CANNES COCKTAIL
Image captionTiger Shroff amesema Stallone ni 'shujaa wake'
Muigizaji nyota India Tiger Shroff ndiye analipokea jukumu hilo kuu.
Kuhusu uamuzi wake wa kuizindua filamu hiyo Cannes, Anand amesema: "Rambo anatambulika katika kila sehemu ya duniani. Kwahivyo ni muhimu kuizundua filamu hiyo katika eneo kuu la utengenezaji Filamu."
Amesema amepata msukumo wa kuitengeneza filamu hiyo Kihindi kutokana na uzito wa muigizaji mkuu "muigizaji wa kikweli wa kupigana aliye na moyo mkubwa", aliyefufuliwa na Stallone.
Anand amesema ameipangilia filamu hiyo kwa namna ambavyo itakuwa rahisi "kueleweka India" - lakini ameonya: " Huenda ikazusha mzozo kama ilivyokuwa kwa Rambo First Blood katika miaka ya 80.
"Inakufanya ufikirie, na inahusu hali inayojiri India na inakuwa tofuati kwa namna hiyo."
Sylvester Stallone tweetHaki miliki ya pichaSYLVESTER STALLONE/TWITTER
Stallone alituma ujumbe katika mtandao wa kijamii wiki iliyopita akisema Rambo ni "mtu sifika", akiongeza : "Nataraji hawato iharibu."
Lakini baadaye alituma ujumbe kwa Shroff mwenyewe akimtakia kila la kheri.
"Ameonesha imani kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter. Ni kama "kuungwa mkono na Mungu mwenyewe," amesema Anand.
Alipoulizwa wanavyofikiria mashabiki wa filamu asili , alisema: " Nafahamu sio mashabiki wote wa Rambo watakaoridhishwa kwa sababu hawataki iharibiwe. Lazima nionyeshe thamani ya maana ya Rambo.
RamboHaki miliki ya pichaGETTY/HULTON
Image captionFilamu asili za miaka 80 za Rambo ziliigwa na Sylvester Stallone kama John Rambo, ambaye alikuwa mpiganaji mkongwe wa vita vya Vietnam
"Filamu aina hizo haizigwi tena, kwahivyo lilinifurahisha kuwaletea vijana."
Shroff, mwenye miaka 27, amesema anahishi mpango huo ni mzuri sana kiasi cha kutoamini alipofuatwa mara ya kwanza .
Alisema: "maishanini mwangu, Sylvester Stallone atasalia kuwa Rambo. NI shujaa wangu.
"Sitaki kuchukuwa mahala pake lakini kutoa mtazamo tofuati kuuhusu. "Ni jukumu kubwa kujitwika."
Filamu hiyo inaanza kuigizwa mwishoni mwa mwaka katika milima ya Himalayas na itapeperushwa mwaka 2018.

source:bbc

Related Posts:

  • Trump kuzuru Israel chini ya ulinzi mkali Rais wa Marekani Donald Trump anazuru Israel na Maeneo ya Wapalestina leo, akiendelea na ziara yake ya kikazi katika maeneo ya Mashariki ya Kati. Atafika maeneo hayo akitokea Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani, amba… Read More
  • Mwanamke akata uume wa kiongozi wa dini India   Mwanamke mmoja wa umri wa miaka 23 nchini India amekata uume ya wa kiongozi mmoja wa dini kwenye jimbo lililo kusini mwa nchi la Kerala, akidai kuwa alimbaka kwa miaka kadha. Polisi wanasema kuwa kiongozi huyo wa d… Read More
  • Libya yakabiliwa na vita vya ndani Taarifa kutoka nchini Libya zinaelez kwamba jeshi liloljitangaza kuwa la taifa hilo, ambalo linaunga mkono mamlaka yenye makao yake katika mji wa mashariki wa Tobruk,limefanya mashambuliuzi kadhaa ya anga dhidi ya vikosi pi… Read More
  • Tamko la mradi wa bomba la mafuta ghafi lasainiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima… Read More
  • Rwanda yaitoza MTN faini ya dola milioni 8 Kampuni kubwa ya mawasiliano ya MTN tawi la Rwanda imetozwa faini ya zaidi ya dolla milioni 8 za Marekani kwa kile kilichotajwa kuwa kukiuka makubaliano baina yake na serikali ya nchi hiyo. Kampuni hiyo yenye wateja takrib… Read More

0 comments:

Post a Comment