Tuesday 23 May 2017

Je unawajua wakongwe waliozoea kufanya kazi duniani?

Prince PhilipHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMwanamfalme Philip anasema atajiuzulu baadaye mwaka huu
Wakati Mwanamfalme Philip, anayeingia miaka 96 mwezi Juni anastaafu majukumu yake ya kifalme baadaye mwaka huu, tunawaangazia baadhi ya watu wanaofurahia kazi zao kiasi cha kuamua kuendelea kufanya kazi,wengi wao hata kumpita Kiongozi huyo wa Edinburgh.
David Goodall, Mwansayansi mkongwe Australia
Mkongwe huyo wa miaka 103 mwaka jana alishinda kesi kuendelea kufanya kazi katika chuo kikuu kilichoko magharibi mwa Australia cha Edith Cowan huko Perth.
Dr Goodall aliagizwa kufanya kazi akiwa nyumbani 2017 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wake, lakini chuo hicho baadaye kilisema, nafasi nzuri imepatikana katika tawi la chuo hicho lililoko karibu na makaazi ya mwanasayansi huyo.
Dr Goodall akifanya kazi katika chuo kikuu cha Edith CowanHaki miliki ya pichaABC
Image captionDr Goodall amechapisha matokeo ya utafiti zaidi ya 100
Dr Goodall, aliyelazimika kuachana na uigizaji, kutokana na kutoweza kuendesha gari kwenda kufanya mazoezi kwasbabau ya matatizo ya kuona, amesema ameshukuru kuwa chuo kikuu hicho kimeweza kumpa nafasi.
"Lakini bado nadhani suala la kuhusu usalama wangu halikustahili kuweko," ameliambia shirika la utangazaji Australia ABC.
Dr Goodall, ambaye sasa anashikilia wadhifa wa mtafiti muandamizi katika chuo hicho, amechapisha zaidi ya nyaraka 100 za utafiti katika ekolojia katika kipindi cha miaka 70.
Anthony Mancinelli, Kinyozi mkongwe duniani
Mkongwe huyu wa miaka 106 kutoka kaunti ya Orange jimboni New York ametuzwa rasmi sifa hiyo na Guinness Book of World Records mnamo 2012.
Lakini Mancinelli, ambaye amekuwa akinyoa nywele kwa zaidi ya miongo 9 anaendelea kufanya kazi.
Anthony Mancinelli akiwa kaziniHaki miliki ya pichaHVNN/YOUTUBE
Image captionAnthony Mancinelli amehudumu kama kinyozi kwa zaidi ya miaka 90
"Usisite. Ukistaafu na umezeeka katika unachokifanya - tafuta kingine cha kufanya. Usistaafu," alisema katika mahojiano hivi karibuni na WCBS 880.
Anakumbuka kwa furaha siku za kwanza alipoanza kufanya kazi dukani ambapo vinyozi walilazimika kutoa huduma nyingine za kuondosha maumivu na hata kutumia ruba kupunguza shinikizo la damu.
Bi Mastanamma - Nyota wa YouTube India
Ana miaka 106 na huwavutia watu wengi kwenye kipindi chake cha upishi India.
Anatumia mbinu rahisi za upishi anazoziita "mbinu za kijijini". Hupika chakula kitamu cha kitamaduni India
PIcha ya Bi Mastanamma kutoka ukurasa wake wa YouTubeHaki miliki ya pichaYOUTUBE
Image captionBi Mastanamma asema mtu yoyote anaweza kupika
Mastanamma, anatoka jimbo la India kusini Andhra Pradesh, na anasema upishi sio mgumu na mtu yoyote anaweza kupika.
Fikra ya kuanzisha kipindi chake ilitokea kwa kitukuu chake aliyechapisha video zake akipika.
Jack Bertrand Weinstein, Jaji wa serikali Marekani
Mkongwe huyu wa miaka 95 anayefanya kazi katika wilaya ya mashariki New York, alipokea wadhifa mkuu mnamo 1993.
Hatahivyo tofauti na majaji wengine wakuu, anafanya kazi kikamilifu.
Jack Bertrand WeinsteinHaki miliki ya pichaUSCOURTS.GOV
Image captionJaji Weinstein: " kila asubuhi huwa nina hamu kubwa kuingia mahakamani".
Alipoulizwa mwaka 2014 kama anafanya kazi kwa saa kamili alijibu: "Ndio, nabeba mzigo kamili kama jaji mwingine yoyote anayefanya kazi katika mahakama hii kwa hiyo unapouliza nimefanya kazi siku ngapi, ni siku saba. Siku ngapi mahakamani? Tano. Ni kazi nzuri mno.
Alihudumu katika jeshi la majini la Marekani wakati wa vita vya pili vya dunia, na alistaafu kama luteni.
Shigeaki Hinohara - Huenda daktari mkongwe zaidi anayefanya kazi kutoka Japan
Mkongwe huyu wa miaka 105 wenzake humtambua kama mali ya kitaifa inayoishi Japan
Dr Hinohara anaongoza taasisi tano kando na kuwa rais wa hospitali ya kimataifa ya St Luke's Tokyo.
Shigeaki HinoharaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDr Hinohara amechapisha maelfu ya nyaraka kuhusu utabibu
Na bado huitembelea hospitali hiyo kila siku kuwakagua wagonjwa.
Babake, ni kiongozi wa dini ya kikristu inaarifiwa alimpa ushauri muhimu: "kuwa na malengo makubwa na uyatimize maishani kwa hikima. Huenda usiyatimize ukiwa hai, lakini usisahau kujaribu, ndipo utaweza kufanikiwa."
Dr Hinohara amechapisha maelfu ya nyaraka ya kitabibu, na ameandika mamia ya vitabu.

source:bbc

0 comments:

Post a Comment