Tuesday, 23 May 2017

Alberto Msando ajiuzulu Ushauri wa chama cha Act-Wazalendo



Mkuu wa Chama Cha Act-Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa mshauri mteule wa Chama hicho Albarto Msando.

"Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo".

Zitto amesema kuwa  Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu  "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.

Related Posts:

  • Mume amuua mkewe kwa kipigo Mwanamke mmoja amekutwa akiwa amefariki dunia chumbani kwake huku mwili wake ukiwa na majeraha baada ya kupigwa na mumewe, wilayani ilemela mkoani Mwanza.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kwamba tuki… Read More
  • Wastara awajia juu wanaomtukana Zari Wastara afunguka kwa Uchungu Kuhusu Zari Kutukanwa:From @wastara84 - Ukimuona nyani kazeeka na bado anaishi ujue kakwepa mishale mingi saana mtanisamehe kwa masamiati huuLakini mim ni mama sijawahi kusahau uchungu wa mwana … Read More
  • Ivan Don Azikwa na Mamilion ya Pesa Kaburini  KUTOKA KWENYE MAZISHI UGANDA...... pesa zaidi ya 30 mil zamwagwa ndani ya kaburi la Ivan Don... Kabla ya maiti kuwekwa....!! Ni balaaaaa..... RIP IVAN DON ila ingekuwa hapa bongo ingebidi hlo kaburi lilindwe hata miez… Read More
  • Awatapeli raia kwakutumia sare za JWTZ Mwanza. Mkazi wa Kitangili, Shinyanga Francis Kilalo  (31)anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli… Read More
  • Spika Ndugai atamani kupanda mabasi ya mwendo kasi Dodoma.  Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anatamani kupanda mabasi ya mwendo wa haraka yaliyoko jijini Dar es Salaam.Pia, ameishauri kampuni ya usafiri ya Udart kuangalia uwezekano wa kuwekeza mjiniDodoma.Akizun… Read More

0 comments:

Post a Comment