Wednesday, 24 May 2017

Trump anakutana na Papa Francis Vatican

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliwasili Roma JumanneHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliwasili Roma Jumanne
Rais Donald Trump anatarajiwa kuzungumza na Papa Francis na viongozi nchini Italia mjini Roma katika awamu ya tatu ya ziara yake baada ya kuingia madarakani.
Trump na kiongozi huyo wa kidini tayari wame tofautiana kiasi kuhusu masuala yakiwemo uhamiaji na mabadiliko ya tabia nchi.
Kiongozi huyo wa Marekani anakutana pia na rais wa Italia na waziri mkuu, kabla ya kuelekea Brussels kwa mkutano wa jumuiya ya kujihami NATO.
Awali aliapa kufanya kila awezalo kuisaidia Israel na Palestina kuidhinisha amani alipokamilisha ziara yake mashariki ya kati.
Pope Francis.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPapa Francis ameshutumu hatua ya rais Trump kujenga ukuta katika mpaka baina ya Mexico na Marekani
Papa Francis na Rais Trump ni viongozi wawili walio na tofauti kubwa.
Upande mmoja Papa ameelekeza maisha yake kutetea maskini na wasiojiweza na upande mwingine mfanyabiashara, Rais Trump amelenga kutajirika na amejihusisha na mabilionea katika baraza lake la mawaziri.
Na licha ya kwamba huu utakuwa mkutano wao wa kwanza, tayari wametofuatiana. Wakati wa uchaguzi, na katika ziara yake katika mpaka wa Mexico na Marekani, Papa Francis amesema watu wanaofikiria tu kujenga ukuta badala ya madaraja sio wakristo.
Donald Trump amesema matamshi hayo ni ya kuaibisha na amemshutumu kiongozi huyo wa kidini kwa kuwa kibaraka cha serikali ya Mexico.
Lakini leo Jumatano wote watapania kuelewana.

Related Posts:

  • Imevujaa!! Kumbe John Bocco alikuwa anahitajika Azam Golikipa namba moja wa Azam FC Aishi Manula amesema, John Bocco ‘Adebayor’ bado alikuwa anahitajika ndani ya kikosi cha Azam. Manula amesema, licha ya timu yake kusajili wachezaji wengi wa kigeni miaka ya hivi karibuni … Read More
  • Kambi ya Upinzani Bungeni uvunjwe MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), amelitaka Bunge kuvunja Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na maoni ya kambi hiyo kutosikilizwa.Lema amedai kuna kuchujwa kwa maneno yanayochangiwa na wabunge w… Read More
  • Daktari wa upasuaji matiti afungwa jela miaka 15  Daktari wa upasuajia wa matiti Ian Paterson amefungwa jela miaka 15 kwa kufanya upasuaji usio muhimu. Paterson, mwenye umri wa miaka 59, aliwafanyia upasuaji wanawake tisa na mwanamume mmoja baada ya kuwadanganya k… Read More
  • BAADA YA KIFO:ndugu wataka uchunguzi kifo cha Ndesamburo Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemone Ndesamburo amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya KCMC, Mkoani humo.Katib… Read More
  • Ndugai amkumbuka kwa majonzi Ndesamburo Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anamkumbuka marehemu Phillemon  Ndesamburo aliyekuwa mbunge wa Moshi  Mjini (Chadema) kwa uchapakazi wake na mapenzi yake makubwa kwa wapiga kura wake.“Nimepokea kwa masikitiko t… Read More

0 comments:

Post a Comment