Saturday, 17 June 2017

Wamiliki wa Makentena ya Magogo yaliyonaswa bandarini kufikishwa Kortini

SERIKALI inaendelea kuchunguza wamiliki wa Makontena matano ya magogo yaliyokamatwa bandarini   mwaka juzi, kuwafikisha  mahakamani.

Shehena hiyo ya magogo ya mti aina ya Mkulungu ilikamatwa Novemba 5, 2015 yakionyesha yanatokea Zambia kwa ajili ya kusafirishwa nchi za Mashariki ya Mbali.

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi ya Rasilimali za Misitu, Mohamed Kilango, alisema makontena hayo yalikamatwa baada ya kukosekana kwa nyaraka za mzigo huo.

“Wale wahusika tuliwaambia watuletee ‘documents’ (nyaraka) wakashindwa. Sasa tulichokifanya ni kuendelea na taratibu za kiserikali ili watu hao wapelekwe kwenye mkondo wa sheria. Uchunguzi bado unaendelea siwezi kusema ulipofikia,” alisema.

“Nyaraka zimeshaletwa lakini zinahitajika kuthibitishwa. Lazima tukubaliane na serikali ya nchi ambazo zimetoka kwani utaratibu wa kimataifa upo ili kujiridhisha. Kwa sasa tuko kwenye hatua nyingine,” aliongeza.

Kilango alisema suala hilo limechukua muda mrefu kwa kuwa linahusisha nchi mbili, hivyo uchunguzi unafanyika kwa nchi zote ili kujiridhisha.

Kilongo alisema kama mtu anasafirisha magogo kwenda nje ya nchi, kuna vitu vitatu ambavyo mhusika anatakiwa kuwa navyo. Alivitaja vitu hivyo kuwa ni cheti cha ubora wa mazao ya nchi, cheti cha  kuruhusiwa kusafirisha mazao katika nchi anayotoka na kibali halisi cha nyaraka.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, alisema nchi hairuhusiwi kusafirisha magogo kwenda nje na kilichoruhusiwa ni mbao kwa kibali maalumu

Related Posts:

  • Dawa za kupunguza makali ya HIV Watafiti nchini Uingereza wanasema dawa za kupunguza makali ya virusi katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini zimeboreshwa kiasi kwamba watu mwenye Virusi vya UKIMWI wanaweza kuishi kwa karibia sawa tu na watu wengine wasio na… Read More
  • Msichana wa Chibok akataa kurudi nyumbani Wasichana wa Chibok Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria. Alitarajiwa kuwa miongoni… Read More
  • Majaribio ya ndege mpya za Boeing yasitishwa Shirika la ndege la Boeing limesitisha kwa muda safari za kufanyia majaribio ndege yake mpya ya 737 MAX kutokana na uwezekano wa kasoro kwenye injini za ndege hizo. Hatua hiyo imechukuliwa siku chache kabla ya shirika hil… Read More
  • Mkurugenzi wa kampuni ya ndege apigwa chapati ya uso Australia Hotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Australia Airline Qantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chapati usoni. Alan Joyce alikuwa akihutubia mkutano wa biashara katika eneo la Perth wakati mtu mmoja alipopand… Read More
  • RATIBA YA LIGI YA AJUCO             AJUCSO MINISRTY OF SPORTS AND ENTERTAINMENT AJUCSO LEAGUE                     &n… Read More

0 comments:

Post a Comment