Wednesday, 7 June 2017

Kuna hofu abiria wote 120 waliokuwa kwenye ndege ya Burma, wamefariki

Ndege ya Mizigo iliyopotea ikiwa na watu 120Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNdege ya Mizigo iliyopotea ikiwa na watu 120
Matumaini yanazidi kufifia kwa abiria wote 120, ambao walikuwa ndani ya ndege moja ya jeshi la Burma, iliyopotea angani ilipokuwa ikipaa katika maeneo ya bahari ya Andaman.
Duru zinasema kuwa, kulikuwa na wanajeshi 106, familia zao na wahudumu 14 wa ndege wakati wa kupotea kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo muundo wa Y8 ya mzigo iliyoundiwa China, ilikuwa imemaliza muda wa nusu saa tangu ilipopaa angani kutoka uwanjani.
Taaarifa za hivi punde zasema kuwa, mabaki ya ndege imeonekana baharini, huku ndege za kijeshi zikiwemo helikopta, zikiendelea kusaka eneo hilo, ili kuokoa manusura.
Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa wakuu wa nchi hiyo.
Ndege hiyo ya kijeshi, ilikuwa ikipaa kati ya Yangon (Rangoon) na mji ulioko kusini mwa nchi hiyo wa Myeik.
Shughuli za kutafuta na kuokoa manusura zinaendelea.
Ramani ya Myanmar ama Burma
Image captionRamani ya Myanmar ama Burma
"Tulipoteza mawasiliano na ndege hiyo mwendo wa saa nne na dakika 35 leo asubuhi saa za Afrika Mashariki [07:05 GMT], pale ndege hiyo ilipofika maili 20 magharibi mwa mji wa Dawei," jeshi la Burma limesema kwa njia ya taarifa.
Awali shirika la habari la AFP lilisema kuwa kulikuwa na abiria 105 na wafanyikazi 11 kwenye ndege hiyo.
Ndege za wanajeshi pamoja na helikopta zimetumwa katika eneo hilo katika shughuli za kuwatafuta manusura au mabaki ya ndege hiyo ambayo kufikia sasa inaaminika kuwa imeanguka.
Taarifa inaongeza kuwa, ndege hiyo ilikuwa angani ikivuka bahari ya Andaman, pale ilipotoweka.

source:bbc

Related Posts:

  • Polisi 4 wauawa katika mlipuko Garissa KenyaHaki miliki ya pichaEPAImage captionMaafisa wa usalama katika shambulio la 2015 ambapo watu 147 waliuawa katika shambulio la al Shabaab dhidi ya chuo kikuu cha Garissa Kenya Maafisa 4 wa polisi wameuawa na wengine 4 kujeruhiw… Read More
  • Manji amethibitisha tena kujiuzulu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amethibitisha kuachia ngazi katika nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo, uamuzi ambao aliuchukua tangu Mei 20, mwaka huu. Kutokana na uamuzi huo wa Manji sasa Yanga itakuwa chin… Read More
  • Trump anakutana na Papa Francis VaticanHaki miliki ya pichaAFPImage captionRais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliwasili Roma Jumanne Rais Donald Trump anatarajiwa kuzungumza na Papa Francis na viongozi nchini Italia mjini Roma katika awamu ya tatu ya ziara … Read More
  • Je unawajua wakongwe waliozoea kufanya kazi duniani?Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionMwanamfalme Philip anasema atajiuzulu baadaye mwaka huu Wakati Mwanamfalme Philip, anayeingia miaka 96 mwezi Juni anastaafu majukumu yake ya kifalme baadaye mwaka huu, tunawaan… Read More
  • Alberto Msando ajiuzulu Ushauri wa chama cha Act-Wazalendo Mkuu wa Chama Cha Act-Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa mshauri mteule wa Chama hicho Albarto Msando."Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Ch… Read More

0 comments:

Post a Comment