Wapiga kura walipokuwa wanafika vituoni kupiga kura Uingereza, mbwa wa kila aina hawakuachwa nyuma.
Na punde si punde, watu walianza kugundua kwamba wanyama hao walikuwa wengi sana ajabu, na kitambulisha mada cha #DogsAtPollingstations (Mbwa vituo vya kupigia kura) kikaanza kuvuma mitandaoni.
Kando na mbwa, kunao watoto, paka na hata nungunugu walionekana na kuvutia watu vituoni.
Wengi walipakia picha za mbwa wao mtandaoni Alhamisi asubuhi na katika kipindi cha saa mbili za kwanza baada ya vituo kufunguliwa, ujumbe 8000 kuhusu mbwa ulikuwa umepakiwa mtandaoni.
Mtindo kama huo ulionekana katika uchaguzi wa mitaa mwezi uliopita, kura ya maoni kuhusu kujiondoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya na wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mwaka huu, Twitter hata walitoa kibonzo cha mbwa akiwa amevalishwa bendera ya Uingereza.
Twitter walishirikiana na wakfu wa The Dogs Trust kutetea kuwepo kwa mazingira bora ya mbwa kwenye vituo vya kupigia kura.
There was an interruption when an unexpected guinea pig popped up.
Lakini mbwa bado walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya mbwa aina ya Pooch hawakuweza kufika vituoni, lakini wanaonekana kutotaka kuachwa nje:
Kuliwepo hata hivyo na wanapaka, na kitambulisha mada ya #catsatpollingstations (paka vituoni) pia kilivuma kiasi.
Hata nungunungu huyu kwa jina Friday alitaka kushiriki Hemel Hempstead.
0 comments:
Post a Comment