Kutokana na mambo mbalimbali ambayo yanaendelea nchini ikiwepo mikataba mibovu ya madini viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamekuwa wakisema njia pekee ya kuweza kusaidia nchi kulinda maliasili zake ni kuwa na Katiba mpya.
Jambo hili limewaibua Wenezi wawili wa vyama vya siasa akiwepo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kutoka Chama Cha Mapinduzi na Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu ambao walinyukana kwa hoja juu ya Katiba mpya huku Humphery Pole Pole yeye akisema kuwa waliofanya katiba ikwame ni viongozi wa upinzani pamoja na viongozi wa CCM ambao waliweka maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya wananchi.
Humphery Pole pole alidai kuwa wao kama Chama Cha Mapinduzi saizi wanajisafisha ili wawe wasafi ndiyo baadaye waje kuzungumzia suala la Katiba Mpya wakiwa ni wasafi na kusema anaamini pia vyama vya upinzani ndiyo vitachelewesha tena kwani wao mikono yao ni michafu lakini haoni dalili za wapinzani hao kujisafisha.
"Katiba hatukufanikiwa kwa sababu wengi wa sisi viongozi tena kutoka upinzani na Chama Cha Mapinduzi tuliweka maslahi yetu mbele tukaweka mbali maslahi ya wananchi kwa sababu za ubinafsi lakini serikali ya CCM saizi tunarekebisha hayo. Mimi nilitegemea na vyama vingine vikianza kuosha mikono yao michafu mno halafu ndiyo tuzungumze katiba, ukizungumza katiba na una mikono michafu haina tofauti na chakula kipo mezani una mikono michafu na bado unataka kula haiwezekani" alisema Pole Pole
Kwa upande wa pili Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu alipingana na hoja ya Pole pole na kusema kuwa analeta hoja nyepesi kwenye jambo la msingi na kusema kuwa katiba ya nchi ni mali ya wananchi na si mali ya chama fulani cha siasa, hivyo kusema CCM saizi inajisafisha ikimaliza kujisafisha ndiyo izungumzie katiba si sawa.
"Ndugu Pole Pole anasema mchakato wa katiba ni sharti tusubiri CCM inawe mikono, kanuni ya wapi hii? Taratibu za wapi hizi za kidunia za kutengeneza katiba zinazosema tunasubiri chama tawala kijisafishe, kinawe mikono kiwe safi ndipo turejee mchakato wetu, taratibu za wapi hizo zinazosema mpaka vyama vya siasa vinawe mikono ndipo virejee mchakato wa katiba. Katiba ni mali ya wananchi na wanasiasa wakizungumza wanazungumza kama sehemu katika jamii, wanasiasa watasema lakini haiondoi ukweli kwamba katiba ni zao la wananchi, kwa hiyo kusema mpaka CCM iwe safi ni kurejea katika propaganda" alisema Ado Shaibu
Mbali na hilo Ado Shaibu alimtaka Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi kutoka CCM ndugu, Humphery Pole Pole kuwa wazi kwamba kwa CCM ya sasa katiba siyo kipaumbele chao hivyo wananchi wajue kuliko kufanya propaganda ili hali anatambua wazi kuwa hata Rais John Pombe Magufuli katiba si ajenda yake kwa sasa.
"Rais Magufuli yeye alishaweka wazi kuwa katiba siyo ajenda yake, sasa kuna dhambi gani wapishi wa propaganda wa CCM kusema kwamba hatutaki katiba siyo vipaumbele vyetu, wanyooshe tu maelezo na si kupindisha pindisha ili watu wajue namna ya kupigania katiba yao" alisisitiza Ado Shaibu
Humphery Pole Pole alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba ambayo iliwasilisha kwenye Bunge rasmi la Katiba.
Friday, 16 June 2017
Home »
» Mvutano waibuka baina ya CCM, ACT- Wazalendo kuhusu katiba mp
Mvutano waibuka baina ya CCM, ACT- Wazalendo kuhusu katiba mp
Related Posts:
Wakimbizi waugua kambini nchini IraqiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMaelfu ya watu wameukimbia mji wa Mosul baada ya kutokea mapigano ya kudhibiti mji huo Mamia ya watu wameugua na mtoto mmoja amepoteza maisha kwa kile kinachoelezwa kutokana na kul… Read More
Kiongozi wa upinzani Urusi atupwa jela kwa kuandaa maandamanoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionAlexei Navalny (kulia) ana nia ya kugombea urais mwaka ujao Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amehukumia kifungo cha siku 30 jela kwa kukiuka sheria baada ya kua… Read More
Mabaki ya binadamu 'wa kwanza' yapatikana MoroccoHaki miliki ya pichaPHILIPP GUNZ/MPI EVA LEIPZIGImage captionUjenzi wa kwanza wa kisukuku cha awali zaidi cha binadamu kutoka Jebel Irhoud (Morocco) kulingana na nakala za tomografia. Uchunguzi umebainisha kuwa dhana ya kuwa … Read More
Rais wa zamani wa Panama Ricardo Martinelli akamatwa MarekaniHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionRicardo Martinelli anakana madai dhidi yake Rais wa zamani wa Panama Ricardo Martinelli amakamatwa katika jimbo la Florida nchini Marekani. Kikosi cha kudumisha sheria nchini Marekani … Read More
Muuza ndizi wa miaka 94 aliyeporwa Indonesia achangiwa pesaHaki miliki ya pichaFACEBOOK: TOMMYREZA CHOKOLATOZImage captionKind-hearted Indonesians reacted to Mr Suratman's plight in a strong show of support Watu nchini Indonesia wameungana kumsaidia mzee mmoja muuza ndizi ambaye anas… Read More
0 comments:
Post a Comment