Wednesday 14 June 2017

HALI TETE:Chenge agoma kuzungumza

Vigogo waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao serikalini wamevunja ukimya.

Vigogo hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi ulipoanza.

Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo, huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo.

0 comments:

Post a Comment