Aliyekuwa golikipa wa vilabu mbalimbali vikubwa Afrika Mashariki ikiwemo Simba, Yanga, Azam, Gor Mahia na Taifa Stars, Ivo Mapunda amevilaumu vilabu vya Simba na Yanga kwa kudharau na kutokuona umuhimu wa michuano ya SportPesa Super Cup
Ivo Mapunda alisema hayo baada ya timu kutoka Kenya Gor Mahia na AFC Leopards kuingia kwenye fainali za michuano hiyo huku Gor Mahia wakichukua ubingwa wa kwanza wa michuano ya SportPesa Super Cup wakati timu za Tanzania Simba na Yanga zikiwa zimetolewa katika hatua ya Robo fainali na nusu fainali.
Golikipa huyo alisema sababu kubwa timu za bongo kushindwa kufanya vyema ni kutokana na kuchezesha wachezaji ambao hawana uzoefu mkubwa ukilinganisha na timu kutoka Kenya ambazo ziliweka umuhimu kwenye michuano hiyo kwa kuleta wachezaji wazoefu.
0 comments:
Post a Comment