Tuesday, 13 June 2017

Diamond afunguka mchango wa Wema Sepetu kwenye ‘Chibu Perfume’.

Msanii wa muziki, Diamond platnumz amefunguka kuuzungumzia mchango wa malkia wa filamu, Wema Sepetu kwenye perfume yake ya ‘Chibu Perfume’.

Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa, yeye na Wema wanakutana na kuongea sana na wakati mwingine hushauriwa mambo mengi ya kibiashara na mwanadada huyo ambae alikuwa mpenzi wake .

“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond.

Muimbaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya Zari na tayari wamefanikiwa kupata watoto wawili.

0 comments:

Post a Comment